|
Mshereheshaji
Sauda Simba Kilumanga akiwakaribisha wageni katika ukumbi wa JB Belmont
jijini Mwanza kwa ajili ya sherehe za utolewaji wa Tuzo kwa Wanahabari
zinazoandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) |
|
Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Tanzania(TANAPA)Paschal
Shelutete akifanya utamburisho wa wageni mbalimbali waliofika katika
shughuli hiyo. |
|
Baadhi ya wageni mbalimbali katika shughuli hiyo. |
|
Meza kuu iliongozwa na Waziri wa Maliasili na Mazingira ,Lazaro Nyarandu. |
|
Waziri Nyarandu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa TANAPA,Ibrahim Mussa. |
|
Mmoja
kati ya wageni waalikwa alikuwa ni Mkurugenzi wa Umoja wa vilabu vya
Waandishi wa Habari nchini ,Abubakar Karsan ambaye alipata nafasi ya
kuzungumza machache. |
|
Kiongozi
wa Majaji waliofanya kazi ya kupitia kazi za Waaandishi
walioshindanishwa na kisha kupatikana washindi Dk Ayoub Rioba
akizungumza namna washindi walivyopatikana na baadae kuwatambulisha
Majaji wenzake. |
|
Majaji walioshiriki kufanya kazi ya kupitia kazi za washiriki . |
|
Wageni mbalimbali wakifutilia shughuli hiyo. |
|
Mgeni
rasmi katika sherehe za utolewaji wa Tuzo zijulikanazo kama TANAPA
Media Award 2013,Waziri wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyarandu ,akiwa
na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Allan
Kijazi,Mkurugenzi wa Utalii na Masoko Ibrahimu Mussa pamoja na Meneja
Ujirani Mwema Ahmed Mbugi tayari kwa zoezi la utolewaji wa TUZO HIZO. |
|
Mgeni
rasmi katika sherehe za utolewaji wa Tuzo zijulikanazo kama TANAPA
Media Award 2013,Waziri wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyarandu akitoa
mfano wa Hundi ya kiasi cha Sh Milioni moja na laki tano kwa mshindi
namba mbili wa uandaaji wa vipindi vya Radio,Humphrey Mgonja wa Radio
SAUT fm. |
|
Mgeni
rasmi katika sherehe za utolewaji wa Tuzo zijulikanazo kama TANAPA
Media Award 2013,Waziri wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyarandu
akikabidhi mfano wa Hundi ya kiasi cha Sh Milioni mbili pamoja na Ngao
kwa mshindi namba moja wa uandaaji wa vipindi vya Radio,David Rwenyagira
wa Radio 5 FM.
|
|
Mgeni
rasmi katika sherehe za utolewaji wa Tuzo zijulikanazo kama TANAPA
Media Award 2013,Waziri wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyarandu akitoa
mfano wa Hundi ya kiasi cha Sh Milioni moja kwa mshindi namba tatu kwa
waandaji wa vipindi vya Televisheni ,Kakuru Msimu wa Star TV.
|
|
Mgeni
rasmi katika sherehe za utolewaji wa Tuzo zijulikanazo kama TANAPA
Media Award 2013,Waziri wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyarandu akitoa
mfano wa Hundi ya kiasi cha Sh Milioni moja kwa mshindi namba tatu
upande wa Magazeti ,Salome Kitomary wa gazeti la Nipashe.
|
|
Mgeni
rasmi katika sherehe za utolewaji wa Tuzo zijulikanazo kama TANAPA
Media Award 2013,Waziri wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyarandu akitoa
mfano wa Hundi ya kiasi cha Sh Milioni moja na laki tano kwa mshindi
namba mbili kwa waandaji wa vipindi vya Televisheni ,Raymond Nyamwihula
wa Star TV. |
|
Mgeni
rasmi katika sherehe za utolewaji wa Tuzo zijulikanazo kama TANAPA
Media Award 2013,Waziri wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyarandu akitoa
mfano wa Hundi ya kiasi cha Sh Milioni mbili pamoja na Ngao kwa mshindi
namba moja kwa waandaji wa vipindi vya Televisheni ,Vedasto Msungu wa
ITV. |
|
Baadae David Rwenyagira alipata nafasi ya kutoa neno la shukrani kwa niaba ya washidi wa tuzo hizo. |
|
Mkurugenzi
mkuu wa Shirika la hifadhi za Taifa ,Tanzania ,Allan Kijazi akitoa neno
na kisha kumkaribisha mgeni rasmi katika shughuli hiyo ,Waziri wa
Maliasili na Utalii,Lazaro Nyarandu. |
|
Mgeni
rasmi katika sherehe za utolewaji wa Tuzo zijulikanazo kama TANAPA
Media Award 2013,Waziri wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyarandu
akitoahotuba yake mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa tuzo. |
|
Mwanamuziki
Nguli wa muziki wa Bendi hapa nchini King kii a.k.a Mzee wa Kitambaa
Cheupe na bendi yake alitoa burudani kwa washindi pamoja na wageni
waalikwa. |
|
Kila mmoja aliweka kitambaa Cheupe juu. |
|
Baadae likafuatia neno la shukrani toka kwa Mkurugenzi wa Utalii na Masoko ,Ibrahimu Mussa. |
|
Mgeni rasmi akapata picha ya pamoja na washindi. |
|
Watu wa Star Tv ,Bernad James,Yvona Kamutu pia walikuwepo kutoa konos,kwa mwenzao Raymond Nyamwihula. |
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii aliyeko jijini Mwanza.