Changamoto
ya mapungufu yaliyotajwa kwenye maandalizi ya vitabu na mitihani ya
kumaliza darasa la saba imepelekea mheshimiwa James Mbatia
kuwa-challenge maprofesa walioko bungeni kuufanya mtihani wa darasa la
saba ambao kwa mujibu wake haufanyiki.
Akitoa
mchango wake bungeni wakati wa mjadala kuhusu bajeti ya wizara ya elimu
na mafunzo ya ufundi ya mwaka 2014/2015, Mbatia amesema alichukua
mtihani wa darasa la saba na kuupeleka kwa professor wa chuo kikuu cha
Dar es Salaam na alimrudishia majibu kuwa mtihani ule haufanyiki.
“Njoo
kwenye mtihani wa hisabati, na mimi napenda sana hisabati. Mheshimiwa
spika, nilipeleka mtihani huu kwa professor wa chuo kikuu cha Dar es
Salaam, mtihani wa darasa la saba. Professor ameniandikia hapa
‘nimetumia muda wa saa mbili na dakika tatu kufanya mtihani huu bila
kuandika majibu kwenye karatasi na mtihani wenyewe haufanyiki.
"Yaani
ni madudu matupu yako kwenye mtihani huu. Nawachallenge wenzangu ambao
ni maprofesa na wengine wanajua hisabati, wafanye mtihani huu waweze
kupata 100/1000 na mimi ntawapa shilingi milioni 10 ndani ya bunge
hili.” Amesema James Mbatia.
Mbatia
aliendelea kuweka msisitizo kuwa angeweza kuuweka mtihani huo kwenye
meza bungeni hapo na professor yeyete ambaye ataweza kuufanya na kupata
100/100 angempa shilingi milioni 10.
Ameukosoa
vikali mpango wa ‘matokeo makubwa sasa’ ambao amedai utekelezaji wake
umegeuka kuwa madudu yanayotisha kwenye elimu ya Tanzania.
“Mheshimiwa
naibu spika haya ni mambo ya kusikitisha, ni mambo ya kutisha. Na nchi
yetu elimu ni dhaifu ya kupindukia. Elimu ni mapigo wa moyo ya taifa.
Mapigo ya moyo yakienda kinyume na utaratibu wake maisha hupotea. Kwa
hiyo uhai wa taifa la Tanzania hupotea kwa sababu tumeshindwa kuwekeza
kwenye elimu. Wanafunzi wetu wanashindwa kufikiri yakinifu. Power of
reasoning katika nchi yetu imekwenda chini sana kwa sababu elimu yetu ni
dhaifu, ni dhaifu ya kutisha.” Ameongeza.
Amependekeza
kuwa ili kupata tiba, bunge limuombe rais Jakaya Kikwete kuunda tume ya
kudumu ya elimu nchini ambayo itakayokuwa inahakikisha ubora wa elimu
na kudhibiti mambo yanayosababisha kutetereka kwa elimu nchini na
amependekeza iitwe ‘Education quality assurance and control’.