DIAMOND ADONDOKA UINGEREZA KU-SHOOT VIDEO MPYA

 



 Mshindi wa tuzo saba za KTMA 2014 Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz aka ‘Chibu’ na Ommy Dimpoz wameondoka Tanzania jana kuelekea nchini Uingereza.
Diamond ame-share baadhi ya picha za safari hiyo akiwa ameongozana na Ommy Dimpoz pamoja na meneja wake Babu Tale.
Licha ya kuwa Platnumz hajasema kilichompelela Uingereza, lakini mpenzi wake Wema Sepetu kupitia ‘You Heard’ ya XXL, amethibitisha kuwa ‘baby’ wake pamoja na mambo mengine lakini pia ameenda kushoot video. Na katika siku nne zilizopita Platnumz aliwaomba radhi mashabiki wake wa Uingereza kwa kushindwa kufika kwaajili ya show iliyokuwa imepangwa kufanyika May 10 na kuahidi kuwa angesafiri siku si nyingi kwenda London kwaajili ya show hiyo. #Rugby7AfterParty… “ Aliandika Instagram.


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post