JANA ilitimia miaka 18 tangu ndugu zetu walipopata ajali na Meli ya MV.
Bukoba 21 May 1996, na wengi kupoteza maisha! Ni tukio kubwa lililoua
watu wengi nchini na kuacha huzuni kubwa kwa Watanzania.
Comment R.I.P kwao ili waendelee kupumzika kwa amani!
Mei
21,1996 katika ziwa Victoria,Mwanza Tanzania meli ya Mv Bukoba ilipata
ajali na zaidi ya watu 800 kupoteza maisha yao.Meli ilizama kilomita 30
kukaribia kutua nanga kwenye bandari ya mwanza ikitokea Bukoba. Meli ikuwa na uwezo wa kubeba idadi ya watu 430.
Kwenye first
and second class orodha ya abiria ilikuwa 443 na kwenye third
class hakukuwepo rekodi yoyote .Takribani 1000 walifariki kwenye ajali
hiyo.
Afrika ya
kusini ilibidi kutoa msaada wa wanamaji wake waje kutusaidia kufanya
uzamiaji wa kina kirefu kwani tulikuwa hatuna hivyo vifaa na
utalaamu(sijui inagharimu kiasi gani kuvipata vifaa na utalaamu)
Meli ilikuwa na ubovu lakini iliruhusiwa kuendelea na kazi kama kawaida.(nani anajali au kuwajibishwa?)
Vifaa vya
uokoaji mfano majaketi(life jacket) n.k na vitu kama hivyo vilikuwepo
vya kutosha?( au hakuna uzembe wa viongozi..ni kazi ya Mungu kama
walivyozoea kusema)
SWALI LA MSINGI!!!!!
hivi
Serikali imeshindwa kutenga japo dakika 3 nchi nzima kusimama
kuwakumbuka ndugu zetu waliotutoka kutokana na uzembe wa watendaji wa
serikali?
Kama wanaweza kukusanya mamilioni kusherekea sherehe za kisiasa inagharimu nini kutoa tamko kuhusu hiyo siku.
Poleni sana wafiwa..tupo pamoja ..mwenyezi Mungu awapumzishe mahala pema peponi woote waliotangulia mbele ya haki.Amina