SHINDANO la Miss Dar City Center limezinduliwa rasmi jana na
linatarajiwa kufanyika mei 24 kwaka huu katika ukumbi ambao utatangazwa baade,
huku likishirikisha warembo 15.
Akizungumza katika uzinduzi huo jana, mratibu wa shindano
hilo, Judith Charles alisema kuwa, mwaka huu shindano hilo litambapwa na vionjo
tofauti tofauti ili kulifanya kuwa la aina yake.
Judith alisema kwamba, wameangalia changamoto zilizotokea kwa
waandaaji wa waliopita wa shindano hilo, ili kuweza kulifanya kuwa na ubora wa
hali ya juu zaidi kuliko ilivyowahi kutokea.
“Tumetumia changamoto ya waandaaji waliopita wa shindano hili
na sisi tumeamua kuliboresha zaidi na hivyo tunaamini kabisa kwamba litakuwa
katika kiwango cha juu zaidi tofauti na uilivyokuwa hapo mwanzo,” alisema
Judith.
Aidha aliongeza kusema kwamba, ana aimani kubwa kwamba Miss
Dar City Center ndiko atakakotokea Miss Tanzania 2014, kwani wamejiandaa kwa
ukamilifu wa hali ya juu.
Judith alisema kwamba ana imani kubwa na matron ambaye pia
ndie mwalimu wa warembo wa shindano hilo, Eshe Rashid kuwa atawapa mafunzo
mazuri zaidi yatakayowezesha kuwa bora zaidi jukwaani.
Pia aliongeza kusema kwamba, zawadi kwa washindi wa shindano
hilo zitakuwa zimeboreshwa zaidi na hivyo ana imani zitavutiwa zaidi na warembo
hao.
Aidha Judith alisema, shindano hilo kwa kiasi kikubwa
linafadhiliwa na Prima, Zanzi, Sky light
band, Clouds FM, Dimond Bureu De Change LTD, gazeti la Jambo leo, Klabu Maisha
ambako warembo wanafanyia mazoezi, blog ya Wananchi, blog ya Father Kidevu,
Hoteli ya JB Belmont na Machapta Production
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia