Kamanda
wa Chadema Arusha, James Ole Milya akiwa na sura ya tabasamu na mkewe
Janeth jioni ya Mei 3, 2014 katika ukumbi wa Botanical Garden- Sakina
ilipofanyika tafrija kusindikiza harusi yao. Blog hii inapenda kutoa
pongezi za dhati kwa waili hao na kuwatakia kila lililo jema katika
maisha yao ya ndoa hadi uzee wao. Mungu Awabariki sana James&Janeth
Kutoka
kushoto, Msanifu Majengo Dudley Mawalla wa MD Consultancy iliyosanifu
Jengo la PPF Plaza linalijengwa mkabala na Kibo Palace Hotel, anafuata
Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mh Freeman Mbowe na kisha Mbunge wa Arusha
Mjini Mh Godbless Lema na mkewe wakiwa wameshika glass zao kwa ajili ya
kutakiana heri na maharusi.
Maharusi wakifurahi na marafiki. Hapa ni picha ya pamoja na mdau Daniel Urioh
Mbunge Lema akilishwa keki na maharusiMsanii wa Injili Christina Shusho akitoa burudani ukumbini hapo
Msanii wa Kimataifa toka Kenya, Solomoni Mukubwa akitoa burudani
Maharusi wakiimba sambamba na msanii Shusho (haonekani pichani) huku MC OJ kutoka Kenya akifanya yake
***************************************
Sherehe
ya kusindikiza harusi ya James Ole Millya na mkewe Bi Janeth ilikuwa ya
kipekee kwa namna mbalimbali ukiachana na idadi kubwa ya watu
waliohudhuria.
Ni sherehe iliyokuwa na mbwembwe za kila namna na vikorombwezo chungu tele.
Utaani wa kisiasa baina ya Chadema anakotoka bwana harusi na CCM anakotoka bi harusi ulikuwa ni kivutio tosha kwa waliohudhuria. Makundi ya vyama vyote yakiwa na viongozi wao wakubwa yalikuwa yakitambiana kwa kushangilia kila walipopata fursa toka kwa MC. Mabaraza ya vijana kwa vyama vyote ndio yaliyotia for a kwa pande zote katika kutambiana. Huku CCM wakiimba “CCM..CCM..” wenzao wa Chadema walikuwa wakionyesha ishara ya vidole vitatu na kuimba “UKAWA…UKAWA” kila alipotambulishwa kiongozi wao ama kuitwa kufanya jambo fulani. Bavicha Arusha waliongozwa na Mwenyekiti wao Noel Olevaroya na Katibu Glory Kaaya.
Kulikuwa na idadi kubwa ya viongozi wa kitaifa na kisiasa. Alikuwepo Mwenyekiti wa Chadema Taifa ambaye pia ni mbunge wa Hai, Mh Freeman Mbowe bila kumsahau Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema na Mh Kihwelu kwa Upande wa Chadema. Walikuwepo pia Mwenyekiti wa CCM Arusha Mh Olenangoye na Mbunge Viti Maalum CCM Mh Catherine Magige. Madiwani Kessy wa Kaloleni, Ally Bananga wa Sombetini na Msofe wa Daraja mbili wote kupitia Chadema walihudhuria.
Viongozi wa kiserikali alikuwepo Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja Kota, bila kumsahahu Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini John Mongela. Mbunge wa Simanjiro anakotokea James Millya, Mh James Ole Sendeka hakuonekana ukumbini hapo pamoja na kuwa alialikwa. Blog hii iliweza kufahamu kuwa takribani watu 10 walialikwa kutoka katika kila kijiji cha Wilaya ya Simanjiro, pengine ndio sababu iliyopelekea James kupewa zawadi ya ng’ombe wengi mno kutoka kwa jamaa zake Maasai.
Upekee haukuishia hapo tu kwani kwa upade wa washereheshaji walikuwepo nguli wawili wa fani hiyo, MC OJ (Alezander Josephat Ole Midimu Sirkion) ambaye ni mchekeshaji kutoka Kenya na aliwahi kuwa Kampeni Meneja wa Raila Odinga, bila kumsahahu Godwin Gondwe kutoka Tanzania.
Burudani haikuishia hapo kwani nyimbo za injili ziliimbwa na wasanii Christina Shusho kutoka Tanzania na Solomoni Mukubwa kutoka Kenya ambao kwa pamoja walikonga nyoyo za wahudhuriaji vilivyo.

Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia