Mama mzazi wa Mtangazaji wa Television ya Taifa (TBC1), Angella Michael Msangi, Marehemu
Mama Misheli Singoye anatazikwa kesho Jumatano Aprili 30, 2014 ambapo
ibada itaanza saa tatu asubuhi katika Kanisa la Pentekoste, Kigamboni na
baada ya hapo safari ya kuelekea kwenye maziko Zinga kwa Awadhi,
Bagamoyo Pwani.
Marehemu
Mama Misheli Singoye alifariki Aprili 26, 2014 katika hospitali ya
Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa.