Ticker

6/recent/ticker-posts

HIFADHI YA WANYAMAPORI YAKABIDHIWA GARI KUDHIBITI UJANGILI

Mwenyekiti wa HoneyGuide Foundation Olekiri Mbai akikabidhi gari aina ya Suzuki Jimmy kwa Mkuu wa Wilaya wa Monduli Iddi Hassan  ikiwa ni msaada wa shirika hilo katika kusaidia hifadhi ya wanyamapori ya Randilen

Na Woinde Shi8zza,Arusha.

Hifadhi ya Wanyamapori ya Randlen Community Wildlife Management iliyoko wilayani Monduli imekabidhiwa gari aina ya Suzuki Jimmy kwa ajili ya kudhibiti vitendo vya ujangili na uharibifu wa mazingira katika hifadhi hiyo ya jamii .

Akipokea gari hilo kutoka Shirika la Honey Guide Mkuu wa Wilaya ya Monduli Iddi Hassan alisema kuwa gari hilo litasaidia juhudi za kupambana na ujangili katika wilaya hiyo ambayo ili kukuza utalii endelevu kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Wilaya hiyo amesema kuwa msaada huo utasaidia kuimarisha shughuli za uhifadhi kwani hifadhi hiyo ni hifadhi pekee inayofanya vizuri katika wilaya hiyo na kunufaisha vijiji tisa  vinavyozunguka hifadhi hiyo.

Iddi alisema kuwa kwasasa wanajipanga katika kuzuia uvunaji holela wa maliasili katika hifadhi pamoja na kuzuia ujangili hivyo msaada huo wa gari utaongeza nguvu katika mapambano dhidi ya ujangili.


Mwenyekiti wa Honey Guide Foundation Olekiri Mbai  amesema kuwa wameamua kutoa msaada huo unaogharimu kiasi cha shilingi milioni 25 ili kusaidia shughuli za uendeshaji wa hifadhi hiyo ya jamii (WMA) katika kuunga mkono juhudi za serikali kuhakikisha kuwa uhifadhi unafanyika kwa namna ambayo unanufaisha wanajamii wa Monduli.

“Kumekua na changamoto ya Hifadhi nyingi kutokuwa na Meneja lakini hifadhi ya Randilen ni hifadhi pekee yenye meneja ambaye anasimamia shughuli zote za utawala hivyo msaada huu wa gari utamsaidia kutekeleza majukumu yake ya kila siku” Alisema Olekiri

Mwenyekiti wa Hifadhi hiyo Daniel Alais  ameshukuru shirika la Honey Guide kwa kutoa msaada huo ambao utasaidia kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya ujangili na uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kurahisisha utendaji kazi wa kila siku.

Post a Comment

0 Comments