Ticker

6/recent/ticker-posts

SABAYA ADAI KESI YA UHUJUMU UCHUMI IMETENGENEZWA

 ARUSHA


Aliyekuwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro,Lengai Ole Sabaya{35} jana aliendelea kujitetea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha na kudai kuwa kesi ya Uhujumu Uchumi aliyofunguliwa na washitakiwa sita ni ya kutengenezwa kwa Misingi ya kisiasa yenye lengo la kumvunjia heshima kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

 

Sabaya alidai hayo wakati akiongozwa na wakili wake Mosses Mahuna mbele ya Hakimu Patricia Kisinda huku akitokwa na machozi kwa kuangua kilio kizimbani wakati akitoa ushahidi na baadae kukaa chini kwa muda alidai waliotengeneza kesi hiyo ni wapambe wa Mmoja wa wagombea ubunge wa Jimbo la Hai aliyekosa Ubunge akidhani kuwa yeye Sabaya ndio aliyemkoshesha ubunge wa Jimbo hilo.

 

Alidai pia kuwa washitakiwa watano katika kesi hiyo hawajui kwani wengine amekutana nao mahakamani na wengine gerezani Kisongo ila mshitakiwa wa tano katika kesi hiyo Silvester Nyengu{26} anamjua kwa kuwa alikuwa mfanyakazi wa Halmashauri ya Hai.

 

Sabaya ambaye ni mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo alidai kuwa hakuna hata shahidi mmoja wa Jamhuri aliyesema katika ushahidi wake kuwa alikwenda katika gereji ya Mfanyabiashara Francis Mrosso kama Mkuu wa Wilaya ya Hai.

 

Ole Sabaya alidai hakuwahi kwenda katika gereji hiyo wala kwenda kushawishi na kuomba rushwa ya shilingi milioni 90 na huenda waliokwenda katika gereji hiyo ni matapeli.

 

Mahuna alimuuliza juu ya mashitaka matano aliyoshitakiwa nayo na wenzake sita,Sabaya alidai kuwa mashitaka hayo ni ya uongo na ya kutengenezwa dhidi yake.

 

Alidai waliokwenda gereji ya Mrosso na kujitambulisha kuwa ni maofisa wa Mamlaka ya Mapato nchini{TRA} na Maofisa wa Usalama wa Taifa{TISS} na kuchukuwa shilingi milioni 90 walikuwa matapeli kwani yeye hakuwepo siku hiyo Jijini Arusha.

 

 

Sabaya na wenzake wanakabiliwa na Mashitaka matano ikiwemo shitaka la  la kwanza la Uhujumu Uchumi linalowakabili washtakiwa wote ilidaiwa kuwa Sabaya akiwa Mtumishi wa Umma yeye na wenzake Januaria 20 mwaka huu ndani ya Jiji la Arusha na Mkoa wa Arusha akiwa na genge lake la Uhalifu alilokuwa akiliongoza katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro akijua wazi kuwa ni Mkuu wa wilaya alitumia vibaya madaraka yake wakati akijua wazi kuifanya hivyo ni kosa kisheria.

 

Shitaka la pili lililokuwa likimkabili Sabaya mwenyewe ilidaiwa kuwa kuwa Januari 20 mwaka huu ndani ya Jiji la Arusha na Mkoa wa Arusha akiwa Mtumishi wa Umma alishiriki kushawishi Rushwa ya shilingi milioni 90 kutoka kwa Mfanyabiashara Maarufu wa Jijini Arusha,Francis Mrosso mkazi wa kwa Mrombo ili aweze kumsadia katika kesi ya jinai ya ukwepaji kodi iliyokuwa ikimkabili wakati akijua wazi kufanya hivyo ni kosa kisheria akiwa mtumishi wa Umma.

 

Shitaka la tatu lililokuwa likimkabili Sabaya ilidaiwa kuwa januari 20 mwaka huu ndani ya Jiji la Arusha na Mkoa wa Arusha aliomba Rushwa ya shilingi milioni 90 kutoka kwa Mrosso mkazi wa Kwa Mrombo Jijini Arusha ili aweze kumsaidia katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya ukwepaji kodi iliyokuwa ikimkabili Mfanyabiashara huyo wakati akijua wazi kufanya hivyo ni kosa kisheria akiwa mtumishi wa Umma katika Wilaya ya Hai.

 

Shitaka la nne la Utakatishaji fedha haramu lililokuwa likiwakabili washtakiwa wote saba kuwa januari 20 mwaka huu ndani ya Jiji la Arusha na Mkoa walichukua fedha shilingi milioni 90 za Mrosso na kwenda kuzifanyia matumizi yasiyokuwa halali kinyume na sheria ya utakatishaji fedha.

 

Shitaka la Tano analotuhumiwa nalo Sabaya ni matumishi mabaya ya madaraka kwani ilidaiwa kuwa januari 22 mwaka huu akijuwa wazi kuwa ni mtumishi wa Umma alitenda makosa kinyume na taratibu na kanuni za utumishi.

Post a Comment

0 Comments