Ticker

6/recent/ticker-posts

TCRA NA POSTA WATAKIWA KUSHIRIKIANA TAASISI ZOTE ZINAZOGUSA SEKTA YA POSTA

 Na Woinde Shizza , ARUSHA


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na Shirika la Posta Tanzania wametakiwa kuanzisha mashirikiano na taasisi zote zinazoigusa Sekta ya Posta ili kuangalia namna bora ya kudhibiti na kuiendeleza sehemu hii ya mawasiliano. 


Hayo yamebainishwa na Naibu waziri wa habari,mawasiliano na teknolojia ya habari Mhandisi Kundo Andrea  wakati akiongea Kwa niaba ya waziri wa habari ,mawasiliano na teknolojia ya habari Nape Mnauye  katika siku ya kilele cha maathimisho ya siku ya posta afrika yaliyofanyika katika viwanja vya makao makuu ya Papu afrika yaliopo mkoani hapa  ambapo aliwaagiza watoa huduma za posta na usafirishaji wa vifurushi na vipeto wawafahamishe wananchi na wateja wao kuhusu huduma wanazoweza kupata wakifika katika maofisi yao.



Alibainisha kuwa teknolojia ya habari imeleta neema kwa Sekta ya Posta kwa sababu kwa kutumia teknolojia hii ipasavyo kutawezesha uanzishwaji wa huduma mpya za posta zinazoendana na mahitaji ya wateja.

 "Nimefurahishwa kusikia neno ‘Smartposta’ ambayo ni sehemu ya ubunifu wa kutumia teknolojia, hatua hii kwa vyovyote inaongeza wateja  wa Shirika la Posta Tanzania na itaongeza mapato ya shirika na Serikali kwa ujumla, Sisi kama Wizara tutafurahishwa tukipata taarifa za mara kwa mara kuhusu maendeleo ya huduma hii na nyingine mpya zinazoanzishwa"Alibainisha

Alisema kuwa serikali ya Tanzania inaungana na nchi zote za Afrika kuadhimisha Siku ya Posta Afrika ikiwa imebeba  kauli mbiu isemayo “Kuimarisha Ushirikiano na Watoa Huduma Wengine wa Sekta ya Posta Afrika”. 

Aidha alitoa ushauri kwa wadau wengine washirikishwe katika sekta hii  pia hususani, TRA (Forodha), LATRA, Viwanja vya Ndege, Mashirika ya Ndege, watoa huduma za fedha na wengineo kwa sababu wana nafasi katika kuboresha mnyororo wa thamani

Alisema Kauli mbiu ya mwaka huu  imejielekeza kuongeza tija katika utoaji huduma za posta hivyo aliwataka  wadau wote kutekeleza kaulimbiu hii kwa vitendo hadi lengo la kuimarisha ushirikiano na watoa huduma wengine wa Sekta ya Posta Afrika lifikiwe.

 Alisema kuwa  juhudi ambazo Sekta ya Posta wanafanya kuelekea mageuzi yanayoletwa na teknolojia ambayo yanabadili mifumo mbalimbali ya kiutendaji ndani ya Mashirika ya  Posta, juhudi hizo nivyema  ziendelezwe kwa kushirikisha wadau wote ili kutimiza kaulimbinu na kukuza Sekta ya Posta ili kutimiza mahitaji ya wateja ,huku wakijielekeza kutoa huduma kwa bidii ili kukuza Sekta hii muhimu.


Kwa upande wake posta masta mkuu wa shirika la posta Tanzania Macrice Mbodo alisema kuwa wamejipanga vema kuendelea kushirikisha wadau wengine Ili kuwezesha Wananchi kupata huduma Bora wanazostaili kwani wadau hao ni muhimu katika mnyororo wa utoaji huduma.

Alisema katika mpango mkakati wa nane wa shirika pamoja na mengine wameweka vipaumbele kwenye usafirishaji fedha na uwakala biashara mtandaoni ,kuimarisha vituo vya huduma pamoja na mifumo ya Tehama lengo likiwa ni kurudisha shirika la posta ilipokusudiwa kuwa wakati Serikali inaanzisha hivyo wataendela na maboresho.



Post a Comment

0 Comments