Na mwandishi wetu
ameipongeza Kamati Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Dr Tulia Ackson Mwansasu kuwa mgombea nafasi ya Uspika katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.
Alisema kuwa tulia ana sifa, uwezo, uzoefu na amedhihirisha uwezo wa kumudu changamoto za kuliongoza Bunge kwa weledi, umahiri na ufanisi.
Alisema kuwa ni vyema wana CCM na Watanzania wote kuungana na kamati kuu ya CCM kwenye uteuzi huu ili kuhakikisha bunge linapata Spika atakayeweza kusimamia utekelezaji kikamilifu wa majukumu ya Bunge
Aidha pia alisema kuwa Dr.Tulia anaweza kuishauri serikali jinsi ya kukabiliana na changamoto za sasa hivi kwani ni mzoefu wa kuendesha bunge Kwa muda mrefu.
Tags
HABAARI