TEMDO YAJA NA SULUHISHO LA SUMU KUVU KATIKA ZAO LA MIHOGO
Tatizo
la kumaliza uwepo wa sumu kuvu
katika zao la muhogo limepatiwa ufumbuzi na
Taasisi ya Uhandisi na Usanifu
Mitambo Tanzania (TEMDO) mara
baada ya kuwabunia wakulima wa zao hiyo mtambo utakao wasaidia kuchakata
zao hilo mara tu baada ya kuvunwa .
Hayo yamebainishwa
na Ofisa wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko Dkt.
Sigisbert Mmasi kutoka Taasisi ya ubunifu na Usanifu mitambi Tanzania (TEMDO)
wakati akiongea katika maonyesho ya 17
ya SIDO Kanda ya kaskazini yanayofanyika katika viwanja vya makumbusho
vilivyopo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha mkoani Arusha
ambapo alisema kuwa mashine hiyo itamkomboa sana mkulima wa zao la muogo
Alisema kuwa Mtambo huu
utakuwa mkombozi kwa wakulima
kwakuwa muhogo ukivunwa unatakiwa uchakatwe mapema maana ukikaa sana unaweza
ukaharibika ,ukatengeneza sumu kuvu ambayo ni Kuvu/ukungu/fangasi
hushambulia mazao mbalimbali ya chakula, ambapo kawaida kuvu hupatikana kwenye
udongo wakati wote katika hali ya vumbi au muhogo huo
ukaharibika ukawa haufai tena kwa matumizi ya binadamu
Alibainisha kuwa temdo kila mwaka wanakuja na kitu kipya
ambacho kitamsaidia mkulima katika
kazi zake pamoja na kutatua
matatizo katika kilimo anachofanya ,na kwa mwaka huu wameamua kumletea mkulima
mtambo huo ambao utamsaidia mkulima kuokoa mazao yake ambayo yalikuwa yakiaribika kutokana na kukosa soko
Alisema kuwa mtambo huo unauwezo wa kuchakata zao la muhogo takribani
tani 12 na wenyewe unakuwa na tani elfu
12000 za muhogo ambapo ukichakata unapata unga takribani tani tatu.
“mtambo huu ni wa kisasa na
unamsaidia mkulima kwa sababu unauwezo wa kuvuna muhogo siku hiyo hiyo na kuchakata siku hiyo hiyo ,na niwaambie ukishavuna muhogo wako
unaumenya unaingiza kwenye mashine
unatengenezwa uji baada ya
apo unawekwa kwenye draya ambayo inasaidia kukausha ule unga wa muhogo
siku hiyo hiyo kwa iyo unapata unga siku hiyo hiyo ,na unaweza kupeleka kwa
walaji siku hiyo hiyo“alibainisha Mmasi
Alisema kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa
ya kutokuwa na mvua kwa kipindi
kirefu mtambo huo utasaidia kuokoa kile
chakula ambacho kilikuwa kinapotea kwa kuoza bure kutokana na kukaa mda mrefu bila kuchakatwa .


0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia