TEMDO YAJA NA MTAMBO WA KISASA WA KUCHAKATA MUHOGO
Ofisa wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Dkt. Sigisbert Mmasi kutoka Taasisi ya ubunifu na Usanifu mitambi Tanzania (TEMDO)akiongea na baadhi ya wananchi waliotembelea banda lao lililopo katika maonyesho ya 17 ya SIDO Kanda ya kaskazini yanayofanyika katika viwanja vya makumbusho vilivyopo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha mkoani Arusha
Na Woinde Shizza , ARUSHA
Taasisi ya uhandisi na usanifu wa mitambo(Temdo) imefanikiwa kubuni teknolojia mbadala ya kukausha zao la miogo kwa muda mfupi huku miogo hiyo ikifanikiwa kubaki na virutubisho ambavyo vinatakiwa
Sasa wakulima wa zao la miogo mara nyingi wanajikuta wakipata hasara kubwa kutokana na zao hilo kuharibika hasa kwenye mchakato wa ukaushaji
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo kwenye maonesho ya SIDO yanayoendelea jijini Arusha Ofisa mahusiano na masoko wa TEMDO Dkt Sixbert Mmasi alisema kuwa teknolojia hiyo ni zao jipya la uvumbuzi ambao kila mwaka taasisi hiyo inabuni
" hapo awali wakulima wa zao la miogo walikuwa wanalazamika kutumia siku nyingi katika kukausha mihogo hali ambayo wakati mwingine inaharibika "alisema
Dkt Mmasi alisema kuwa uwepo wa teknolojia utaweza kuwaraisishia kazi wakulima wakati wa usindikaji kwani watalazimika kutumia siku moja pekee tofauti na hapo awalia ambapo walikuwa wanatumia siku zaidi ya 10 Huku wakitumia nishati kama jua kama chanzo Cha ukaushaji
"Kwa kutumia teknolojia hii mkulima ataweza kuvuna mhogo wake na akaukausha siku hiyo hiyo na akaweza kufungasja unga katika vifungashio tayari kwa matumizi ya nyumbani Mimi nadhani kuwa huyu ni mkombozi mkubwa sana na Sasa tutaweza kutoa thamani halisi ya zao Hilo la mhogo"alisema
Katika hatua nyingine aliwataka wajasirimali ambao ni wamiliki wa viwanda kuhakikisha kuwa wanatumia uwepo wa taasisi hiyo hasa katika uvumbuzi wa mashine na teknolojia mpya ambazo zote zinalenga kuinua uchumi wa taifa
Alisema kuwa huwa wanawawezesha wadau wa viwanda kwa kuwapa elimu na namna sahihi ya kutumia mashine kwa ajili ya matumizi mbalimbali ndani ya viwanda.
"Lengo letu ni kuona kuwa sekta hasa ya viwanda inakuwa na mapinduzi makubwa kwa kuwa tuna uwezo mkubwa sana wa kutengeneza vitu ambavyo hapo awali vilikuwa vinazalishwa nje ya nchi Sasa tunazalisha na kubuni kwa umairi mkubwa,niwatake watanzania na wamiliki wa viwanda Sasa kutumia taasisi hii ili tubuni wote kwa pamoja.


0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia