ZIJUE BAADHI YA SABABU ZINAZOSABABISHA UGUMBA KWA MWANAMKE
'tatizo la ndoa nyingi kuvunjika na wanawake kukosa watoto,linaongezeka kadri siku zinavyozidi kwenda.
Tatizo la Ndoa nyingi kuvunjika na wanawake kukosa watoto, linaongezeka kadri siku zinavyozidi kwenda , watu mbalimbali wanaelezea baadhi ya sababu zinazofanya watu hao kukosa watoto huku wengine wakisema ni vyakula vinavyoliwa na wanawake kwa kipindi hichi huku baadhi wakibainisha ni wasichana au wanawake kutoa mimba , kutumia madawa ya uzazi wa mpango angali bado mabinti wadogo .
utafiti unaonyesha katika kila ndoa tano au mahusiano matano ya
kimapenzi basi uhusiano mmoja una matatizo ya uzazi hasa ya kushindwa
kuzaa.
hali hii imekua ikiongezeka kadri miaka inavyozidi kwenda mbele kwa sababu mbalimbali kama
mionzi ya mawasiliano yaani wi-fi , magonjwa mapya ya binadamu kwa wanawake utafiti mpya unasema uwezo wao wa
kubeba mimba unaanza kupungua baada ya miaka 30 ya umri kutokana na kuanza
kuishiwa nguvu kwa viungo vya uzazi.
Mwanamama mmoja ambaye anatoa dawa za asili za uzazi pamoja na
zingine anaelezea baadhi ya sababu zinazofanya wanawake wengi kukosa
watoto ambapo anafafanua kuwa moja wapo ya sababu ni pamoja na
kutumia madawa ya uzazi wa mpango katika umri mdogo
Rose Roberty (change Muja) ni mwanamke ambaye anajishughulisha na
utoaji wa dawa za miti shamba kwa wanawake pamoja na dawa zingine
mbalimbali anaeleza sababu kubwa zinazofanya wanawake wengi
kutopata watoto wanapoingia katika ndoa au wanapofikia katika kipindi cha
kutafuta mtoto
-Ulaji wa madawa ya uzazi wa mpango
Rose Roberty (change Muja) anasema kuwa kwa kipindi cha sasa hivi
wasichana wengi wanajiingiza katika swala la kufanya ngono nje ya ndoa hali
ambayo inawapelekea kujiingiza katika matumizi ya dawa za uzazi wa mpango
kabla ya muda wake
‘’mimi na tembelewa na wanawake wengi wakiwa wanatafuta watoto unakuta
mtu amekaa kwenye ndoa mwaka ajapata mtoto anakuja kunywa dawa hizi za
miti shamba baadhi yao wanabahatika wanapata na baadhi hawapati lakini
ukifuata historia yao ya nyumba unawapo wauliza wengi wao wanadai
walikuwa wanatumia vidonge vya uzazi wa mpango mara tu walipoanza sekondari “
“wanasema kuwa imewalazimu kutumia kutokana na kujiingiza katika
tendo la ndoa kipindi wakiwa na umri mdogo sana, na wengine
ukifuatilia historia yao wanakwambia walitoa mimba walivyokuwa
shuleni ,
Anasema kwa sasa mfano binti anamiaka 15 anaenda kutoa mimba
kwakweli wengine wanatumia njia salama ambayo ni hospitali huku wengine
wakitumia njia za asili
Anabainisha kuwa hata njia ya hospitali ya utoaji wa mimba katika
umri mdogo nayo niseme tu sio ya uhakika sana maana katika kuchokonolowa
unaweza kuguswa kizazi na ndio kikaharibika kabisa hali ambayo inamfanya
mwanamke huyo ata akiingia kwenye ndoa kushidwa kubeba mimba
-kujiingiza mahusiano ya ngono wakiwa wadogo
Anaenda mbali na
kubainisha katika kipichi cha zamani watoto wa kike, walikuwa
hawajiingizi katika matendo ya ngono katika umri mdogo lakini kwa kipindi cha
sasa wanawake wengi wamekuwa wakijiingiza katika matendo hayo,
wakiwa na umri mdogo hali ambayo inapelekea kizazi kuanza kusumbuliwa
kikiwa bado hakija komaa vyema
“nitoe mfano tu wa hawa mabinti zetu kwakweli wanavyoanza
kufanya mapenzi wakiwa wadogo unakuta mtoto wa miaka 13 anatembea na mbaba wa
miaka 30 kweli apo ndugu mwandishi hata ukiangalia wanaendana sindo
akimuingilia uyu mwanamke sindio anasogeza kizazi kabisa sasa apo ndio
kamfanya mpenzi wake akishatumika vya kutosha hadi anafikia umri wa kuolewa
si anakuta kizazi kimeisha hakipo karibu kabisa ndio wanakuja
kutafuta watoto hapo baadae mpaka wanafukuzwa kwenye ndoa, alafu wanaanza
kulalamika bure kuwa wamelogwa au ni MUNGU, wewe angalia tu wanaokimbilia
kwenye makanisa ukichunguza historia zao utashangaa”
ATOA USHAURI
Aidha Bi.Rose aliwashauri wasichana ambao ni wanawake kuacha
kutumia vidonge vya uzazi wampango kabla hawaja zaa au kabla
ya kufikia kipindi chake kwani kufanya hivyo kutawaletea madhara makubwa sana
hapo baada
Aliongeza kuwa pia ni vyema wakaacha kutoa mimba haswa katika
kipindi wanapo kuwa na umri mdogo kwani wengi wao ndio wanapoelekea
kupata matatizo ya kukosa mtoto ,ambapo pia aliwataka kuacha kuwa
na tamaa ambazo ndio zinawapelekea kutembea na watu waliowazidi mri ambao
baada ya kufanya nao mapenzi wanawaharibu na kuwasababishia matatizo hapo
baada.
MTAALAMU WA AFYA AELEZEA VYEMA NINI MAANA YA UGUMBA
Brenda Charles ni muuguzi wa kituo cha afya cha Kaloleni aelezea
nini maana halisi ya ugumba nanini
kinasababisha
-Ugumba ni nini
Hii ni hali ya wapenzi au
mke na mume kutopata ujauzito baada ya kushiriki tendo la ndoa bila kutumia kinga kwa muda wa mwaka mmoja
mfululizo.
-Aina za ugumba
unaweza kua wa aina mbili ya kwanza ni ile ijulikanayo
kama primary infertility yaani mtu
hajawahi kubeba mimba kabisa tangu azaliwe na ya pili ni secondary infertility hii ni ile ya mtu ambaye amewahi kuzaa lakini
kwa sasa ameshindwa kubeba ujauzito.
Aidha ugumba una vyanzo vingi ambavyo vingine havifahamiki
mpaka lakini ngoja
niwaeleze baadhi ya vyanzo hivyo.
·
utoaji wa mimba
Huenda hichi ndio kitakua chanzo kikuu cha ugumba miaka ijayo
kwani siku hizi kila karibia kila mwanamke ana sababu za kutoa mimba, utoaji wa
mimba una hatari nyingi ambazo huweza kuleta ugumba kama kuoza au kuharibika
kwa kizazi baada ya kushambuliwa na bakteria, makovu yanayoletwa na vifaa
vinavyotumika kutoa mimba kwenye mfuko wa uzazi na mlango wa uzazi huweza
kusababisha ugumba usiotibika.
·
matatizo ya vizaalishaji vya
mayai [ovari]
ovari ni kiungo ambacho
kinatoa yai moja kila mwezi ili liweze kurutubishwa na mbegu ya mwanaume lakini
kuna magonjwa ambayo yanaweza kusababisha ovari hiyo ikaugua na
kushindwa kutoa mayai, mwanamke ana ovari mbili lakini moja ikiuugua
tu na nyingine haifanyi kazi mfano ugonjwa wa ovarian cyst.
·
matatizo ya mirija ya uzazi
ovari zimeunganishwa kwenye mirija ambayo hupitisha mayai
kwenda kwenye mfuko wa uzazi ,wakati mwingine mirija hiyo huziba kwa sababu
mbalimbali hivyo mayai hushindwa kupita na kusababisha ugumba ,mfano
ugonjwa wa endometriosis, upasuaji na peritonitis.
·
matatizo ya kizazi
kizazi ndio sehemu kuu ambayo mtoto hutunzwa na kuishi kwa miezi
yote tisa, tatizo lolote linaloshambulia kizazi huleta ugumba, mfano, makovu
ndani ya kizazi, uvimbe ndani ya kizazi, kugeuka kwa kizazi na magonjwa ya
zinaa kama kaswende na kadhalika.
·
Kansa
kansa ya kizazi huzuia yai la mama lililorutubishwa
kushindwa kujiweka kwenye kizazi ili kukua, hivyo huchangia sana mimba
kuharibika au kutotungwa kabisa.
·
matatizo ya mlango wa uzazi
oparesheni za kizazi, utoaji wa mimba na magonjwa ya zinaa
huweza kusababisha kuziba kwa mlango wa uzazi hivyo mbegu za kiume kushindwa
kabisa kupita kwenye mlango wa uzazi na kusababisha ugumba.
·
magonjwa mengine ya mwili
magonjwa yeyote ya
binadamu ambayo huingilia mfumo wa homoni za uzazi huleta
ugumba mfano magonjwa ya ini,kisukari, hyperthyrodism, na kadhalika.
·
matumizi ya sigara na pombe
unywaji wa pombe sana na uvutaji wa bangi huzuia yai
kutoka kwenye ovari, lakini pia uvutaji wa sigara hupunguza uwezo wa yai
kutembea kutoka kwenye ovari kwenda kwenye mfuko wa uzazi na wakati mwingine
husababisha mimba kutunga nje ya kizazi.
·
msongo mkubwa wa mawazo
ukiwa unatafuta mtoto
tayari ukiwa umepaniki kwamba huenda usimpate husababisha inasababisha mwili
kutoa homoni kitaalamu kama cortisol ambazo huzuia kazi za homoni za uzazi
kitaalamu kama gonadotrophin releasing hormone hivyo hali huzidi kua
mbaya.
·
uzito uliopitiliza
mwili mkubwa unaingilia mfumo wa utengenezaji
homoni za uzazi hivyo huweza kuleta ugumba katika umri mdogo sana, hivyo
kupunguza uzito ni moja ya njia bora kabisa ya kujiweka kwenye mazingira mazuri
ya kuzuia ugumba.
· Maambukizi Ya Wadudu
Maambukizi ya virusi na bacteria yanayoenezwa kwa ngono
husababisha makovu na uharibifu, kwa mfano, maambukizi ya Hydrosalpnix
yanayosababisha mirija ya uzazi kuziba pande zote na kujaa maji .
· Magonjwa ya Tumbo
Magonjwa ya appendicitis na colitis huleta
madhara kwenye tumbo ambayo yanayoweza kuiathiri mirija ya uazazi kwa kujenga
makovu au kuiziba.
· Upasuaji
Hii ni sababu kubwa ya magonjwa na uharibifu
wa mirija ya uzazi. Upasuaji wa kwenye maeneo ya kinena na tumbo huweza
kusababisha uharibifu utakaozuia upitaji wa yai.
· Matatizo Ya Kuzaliwa Nayo
Mara chache huweza kutokea kuwa mwanamke
akazaliwa akiwa na dosari katika mirija yake ya uzazi.
USHAURI WAKE NINI
Aliwataka wanawake kabla hawajaanza kuzunguka kwa waganga wa
kienyeji na hospitalini ni bora kujichunguza kwa makini kama wako kwenye hatari zinazoelezewa na
kubainisha kuwa hakuna dawa moja ambayo
ina uwezo wa kutibu ugumba kwa watu wote bila kutibu chanzo chake kwanza
Alisema kuwa kila mtu ana dawa yake ya ugumba kulingana na
historia ya maisha yake na chanzo cha tatizo lake, pia wapo wanaoweza kupona
kabisa kulingana na chanzo cha tatizo na hali ya ugonjwa ilivyo pia wapo wasioweza kupona kabisa kama ugonjwa
umesha kaa sana
Aidha aliwataka
wanawake hususani mabinti kuacha baadhi ya tabia ambazo zimeainishwa ili kuepuka na tatizo hili la ugumba.
Elimu ya madhara ya
utoaji mimba katika umri mdogo itolewe ili tatizo hilo liweze kumalizika kabisa
.
habari hii imeandikwa na mwandishi wa habari Woinde Shizza
.jpg)




0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia