WADAU WA UTALII NA UTAMADUNI YATUMIENI MATAMASHA KUKUZA UTALII NCHINI GEKUL
Naibu Waziri wa Utamaduni
Sanaa na Michezo Pauline Gekul amewataka wadau wa Utamaduni na Utalii
nchini kuyatumia kimkakati matamasha ya Utamaduni yanayoendelea nchini
kwa lengo la kukuza Utalii.
Gekul
ameyasema hayo alipokuwa Mgeni Rasmi wakati akizindua Tamasha la Maasai
Festival linalotaraji kufanyika mwezi wa nane mwakani Jijini Arusha
ambapo ameipongeza Taasisi hiyo kwa ubunifu na kukuza utalii.
Amesema
kwamba wakati huu ni muafaka kwa wadau kuungana na serikali katika
kuongeza mazao ya Utalii hapa nchini kwa kuongeza thamani ya shughuli
mbalimbali za Utamaduni na Sanaa zenye upekee ikiwemo za Utamaduni wa
Kimaasai kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi.
"Serikali
ya awamu ya sita inathamini juhudi za wadau mbalimbali za kutumia
shughuli za Utamaduni na Sanaa kwa ajili ya maendeleo ya sekta nyingine
ndio maana Rais Samia alielekeza Tarehe 22 January akiwa Moshi serikali
na wadau kuyatumia matamasha kimkakati kukuza Utalii"
Awali
akitoa Salamu za wizara hiyo Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Pindi
Chana amesema kwamba Maasai Festival ni bidhaa muhimu ya Utalii katika
soko la hapa nchini na waandaaji wamethibitisha hilo kwa vitendo kwamba
Utamaduni na Utalii ni kama bidhaa Moja.
Aidha
aliwashukuru waandaaji hao wa Maasai Festival kwa kuendelea kukuza na
kuimarisha sekta mtambuka kwani Tanzania ni Moja ya mataifa yaliotajwa
kuwa na utajiri wa kipekee katika sekta ya Utamaduni na malikale.
Kwa
Upande wake Mkurugenzi wa Wonderland Afrika na View Point Adventures
Safaris LTD Said Maulid amesema kwamba zaidi ya wageni 1500 kutoka
mataifa ya Ulaya wanatarajiwa kishiriki Tamasha hilo litakaloenda na
matukio manne.
Ameyataja
Matukio hayo ni pamoja na Warsha,Ukimbiaji wa mbio(Maasai Jogging
Bonanza) Onyesho la Mavazi(Maasai Fashion Night) na Maasai Festival CSR
yote hayo yatakuwa ni matukio yatayofanyika katika Tamasha la Maasai
Festival mwakani mwezi wa nane.
"Natoa
wito kwa wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais wetu
Mpendwa Samia Suluhu Hassan kwani tunaona Royal Tour imejibu hivyo
tuanzishe na kujenga ubunifu wa kuanzisha matamasha na bidhaa za Utalii
na Utamaduni zitakazosaidia kutangaza nchi yetu kama alivyofanya Rais
wetu"
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia