- “Sina haja ya kuolewa, nin
achofikiria kwa sasa nipate mtoto wangu mmoja, hawezi kunishinda kumlea na kumhudumia kwa kila kitu, hayo masuala ya kuolewa tuwaachie wenye vipaji vyao, kwa ninayoyasikia najiona kabisa sitawezana na mwanamume,” alisikika msichana mmoja katika mazungumzo yaliyowahusisha wanawake waliokuwa saluni.
Haya ni mawazo wa wasichana au wanawake wengi wa sasa, wakiamini ukuaji wa mtoto unahusisha mahitaji yanayogharimu fedha pekee na ndiyo sababu kumekuwa na ongezeko la malezi ya mzazi mmoja, wengi wao wakiwa wanawake.
Kwa mujibu wa wanasaikolojia, kuwa mama bora hakubagui mwanamke yeyote, haijalishi wewe ni tajiri, maskini, umeolewa, unafanya kazi bali wote wanapaswa kuzingatia majukumu yao katika malezi.
Lakini ulezi hubadilika kulingana na asili na mahitaji ya mtoto, lakini kwa ufupi, kuwa mama bora ni muhimu kwa wote.
Tofauti na ilivyokuwa miaka ya zamani, watoto walipatikana ndani ya ndoa na kulelewa na wanawake waliotekeleza vyema jukumu lao kwenye malezi, sasa hivi msichana mwenye uwezo wa kumudu maisha yake na matamanio ya kupata mtoto anaweza kuamua kuzaa.
Hii ndiyo sababu siku hizi kuwa na mtoto imekuwa miongoni mwa fasheni kwa wadada wasichana, wakiwaza kuwavalisha nguo za kuvutia na kupiga nao picha, suala la malezi sio kipaumbele kwenye vichwa vyao.
Akizungumzia hilo, Dorothy Alfredy (75) anasema suala la malezi ya mtoto, hasa anapokuwa mchanga si rahisi kama mabinti wengi wanavyoamini na ndiyo sababu hata ukuaji wa watoto wengi una dosari za hapa na pale.
Anasema kwa uzoefu alionao mama ana nafasi kubwa katika malezi ya mtoto kwa kumtengeneza katika misingi inayofaa na ili kufanikisha hilo ni lazima awe mstari wa mbele kwenye utekelezaji wa jukumu hilo na sio kuacha kwa watu wengine.
Dorothy anasema wazazi wa zamani walikuwa na muda wa kutosha kulea watoto, tofauti na ilivyo sasa wanawake wakijitahidi kufanya jukumu hilo kwa kikamilifu ni miezi mitatu ya mwanzo tangu ajifungue.
Siku hizi kinamama nao wanafanya kazi na shughuli nyingine za kujitafutia kipato, lakini hili halibadilishi ukweli kwamba msingi mkubwa wa malezi ya mtoto upo kwa mama. Mama ndiye mwenye jukumu la uangalizi wa mtoto na kufuatilia ukuaji wake kuanzia dakika anatoka tumboni hadi pale atakapojielewa na kuweza kujisimamia mwenyewe,” anasema Dorothy.
“Zamani wamama wengi walikuwa wapo tu nyumbani, jukumu kubwa ni kutunza familia na kulea watoto na ndiyo maana naweza kusema watoto walilelewa vizuri na hata ukuaji wao ulikuwa mzuri, siku hizi mama akimaliza ile miezi mitatu ya likizo ya uzazi ndiyo basi, jukumu linahamia kwa dada wa kazi, hii si sahihi.”
Dorothy anasema kwa asili kuna uhusiano mkubwa wa ukuaji mtoto mwenye afya njema na ukaribu wa mama, hilo linasaidia pia kutengeneza upendo kati yao na humfanya mtoto ajihisi yupo katika mazingira salama.
“Kitu ambacho labda hawakifahamu mabinti wa sasa ni kwamba kuwa mama si kazi rahisi, lazima ujitoe hasa katika kufanikisha jukumu hilo, huwa nashangaa mama anashinda kutwa nzima hajamuona mtoto wake, nina mjukuu wangu binti ana kitoto chake naweza kusema kwa kiasi kikubwa yule mtoto analelewa na dada wa kazi.
“Mama kutwa kucha yupo kazini, inaweza ikatokea muda wa mapumziko ndiyo utasikia siku hiyo mara vicoba mara sijui kwenye party gani, mara wenzie wamemfuata anaondoka nao, kwa kifupi hana muda wa kutulia akalea mtoto wake,” anasema Dorothy.
Mhudumu katika wodi ya wazazi, Mariam Mlawa ambaye amefanya kazi kama mkunga anasema mfumo wa maisha na utandawazi umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa mabinti kushindwa kufuatilia maendeleo na ukuaji sio tu wa ujauzito, bali hata watoto wanapozaliwa.
Mariam anasema athari za mfumo mbovu wa maisha haziishii tu kwa mtoto akiwa tumboni, makosa hayo yanaendelea kufanyika hata pale anapozaliwa, akieleza wanawake wengi wa sasa hawataki kula vyakula vinavyotengeneza maziwa kwa hofu ya kunenepa.
Kwa uzoefu wake wa zaidi ya miaka 30 kwenye fani hiyo, amebaini kuwa sasa hivi mwenendo umebadilika na kumekuwa na ongezeko kubwa la wanawake wanaoshindwa kunyonyesha watoto katika siku zao za awali baada ya kuzaliwa, kwa kile wanachodai maziwa hayatoki.
“Siku hizi utasikia wanawake wengi, hasa hawa wasichana wanaojifunga anakwambia maziwa hayatoki, ukifuatilia utagundua hali vile vyakula vinavyoweza kutengeneza maziwa na mtoto akanyonya akashiba. Mabinti wa sasa wanashangaza kwa kweli, analalamika maziwa hayatoki halafu hataki supu wala mitori kwa kuhofia kunenepa. Umewahi kusikia wapi mzazi anafanya diet, haya ni maajabu waliyonayo wazazi wa miaka hii,” anasema mkunga huyo. “Kama huli chakula vizuri ukashiba ni kweli maziwa yanaweza yasitoke au yasiwe mazito ya kutosha kumshibisha mtoto.
Vilevile suala la maziwa kutotoka ni la kisaikolojia, kama kichwani mwako umeiruhusu hali hiyo ni kweli hayatatoka, ila kama unaamua kupambana maziwa yatoke kwa kuanzia kwenye kula na saikolojia yako kuruhusu yatoke basi yatatoka.”
Gladness Mbise (26) ni mama wa mtoto mmoja, anakiri kuwa alipata mtoto huyo akiwa bado hajajiandaa vyema kubeba jukumu la malezi, lakini amelazimika kumtunza kwa kuwa alitamani.
“Nilikuwa natamani kuwa na mtoto, nikiona rafiki zangu wameolewa wana watoto wao nilitamani mno, pamoja na matamanio hayo sikuwa nimejiandaa kubeba jukumu la malezi na ikatokea nikapata ujauzito.
.jpg)
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia