MABINTI WA JAMII YA KIFUGAJI WASHUHUDIA NAMNA WALIVYOKIMBIA KUFANYIWA UKEKETAJI
Kaskazinimwa Tanzania, binti mdogo mwenye umri wa miaka 19, analazimika kutoroka nyumbani, akiacha wazazi, ndugu namarafiki zake.
Upendo (19 )kutoka katika Kijiji cha Olon'goswa wilayani Monduli hayuko peke yake, Msichana mwingine Nanyori (22) aliekua mkazi wa kata ya Musa ya wilayani Arumeru mkoani Arusha naye pia alilazimika kukimbia nyumbani.
Je nini kiliwakuta?
Kujua visa hivi na vingine vingi, nilitembelea mradi wa HealthIntegrated Multisectoral Development (HIMD).
Meneja mradi wa taasisi HIMD Bi.Wendy Brenda akionyesha aina za ukeketaji
Napokewa na Meneja Miradi wa taasisi hiyo isikuwa ya kiserikali, Bi Wendy Brenda, Bila kuuma maneno, Bi Wendy alisema chanzo cha mabinti hao na wengine kukimbia familia, shule na vijiji vyakwao ni Ukeketaji.
Makala hii fupi inaeleza kwa kina visa hivi, ukubwa watatizo nanini kifanyike ilikuwanusuru wasichana hawa na wengine.
-UKEKETAJI NINI
Meneja wamradi wa Health Integrated Multisectoral Development (HIMD), Wendy Brenda anasema kuwa Ukeketaji unahusisha uondoaji wa sehemu au sehemu yote ya siri ya nje ya mwanamke au kuweka jeraha lingine kwa viungo vya uzazi vya mwanamke kwa sababu zisizo za kimatibabu na hakina faida yeyote ya kiafya kwa wasichana na wanawake.
AINA ZA UKEKETAJI
Kuna aina zaidi ya tano za ukeketaji. Kwanza ni uondoaji wa sehemu au kinembe chote
-(sehemu ya nje na inayoonekana ya kisimi, ambayo ni sehemu nyeti/siri ya mwanamke), au mkunjo wa ngozi unaozunguka sehemu ya siri ya mwanamke.
Aina nyingine ni uondoaji wa sehemu au kisimi chote unaweza kusema mikunjo ya ndani ya uke ,au kuacha kuondolewa kwa labia kubwa yaani mikunjo ya nje ya ngozi ya uke ,aina ya tatu inajulikana kama infibulation, hii ni kupunguza kwa mwanya wa sehemu ya uke kupitia utengenezaji wa muhuri wa kufunika sehemu hiyo.
Muhuri hetengenezwa kwa kukata na kuweka upya labia ndogo, au labia kubwa, wakati mwingine kwa kushona, na au bila kuondolewa kwa kisimi yaani kinembe aina nyingine ni ile inajumuisha taratibu zingine zote zenye madhara kwa sehemu ya siri ya mwanamke kwa madhumuni yasiyo ya matibabu, kama kutoboa, kuvuta, kuchanja, kukwarua na kuchoma sehemu za siri.
Aidha pia Kuna aina ingine ambayo wameibua Sasa ivi hii ni Ile ya kukeketa watoto wachanga ambao wamezaliwa jambo ambalo ni baya haswa Kwa mtoto huyo wa kike na hii wanafanya kutokana na kile kinachodaiwa wanaogopa serikali kujua wanafanya tukio hili
MADHARA YATOKANAYO NA UKEKETAJI
Wendy, alibainisha kuwa madhara ya ukeketaji ni pamoja na kusababisha kutokwa na damu nyingi na matatizo ya kukojoa bila kukoma(Vistula), uvimbe, maambukizo ya maradhi kama vile ukimwi kutokana na vifaa ambavyo ngariba anavitumia pamoja na kushidwa kujiamini
Aidha pia alibainisha pia kufanyiwa Kwa kitendo hichi kunaweza kusababishia yule aliefanyiwa kitendo hicho kupata matatizo wakati wa kujifungua wakati mungine kupelekea kuongezeka hatari ya vifo vya watoto atakao wazaa afya yao
kisakolojia, kimahusiano na afya ya uzazi
WALIOKIMBIA KUFANYIWA UKEKETAJI WAELEZA YALIYOWASIBU
Msichana pendo akisimulia yaliyomsibu
Msichana upendo (16 )kutoka katika Kijiji cha olon'goswa wilayani Monduli ni binti aliyekimbia kufanyiwa ukeketaji ambapo aliieleza libeneke la kaskazini blog kuwa akitaka kufanyiwa tukio hilo akiwa darasa la sita .
"Mimi nilikuwa darasa la sita mama akanifata akaniambia ninatakiwa kukeketwa nilikata alinilazimisha na kuniambia lazima nikeketwe kwakuwa Mila zetu ndio zinavyosema na kusema kuwa nisipofanyiwa tohara nitategwa na jamii kwani wasichana wengi wa kabila letu haswa eneo letu wamefanyiwa ,mbali na hivyo dada yangu nae alinifata na kunishawishi na kuniambia nifanyiwe hivyo kwani ata yeye aliefanyiwa na ajapata mazara yeyote kwakuwa Mimi nilikuwa nilishafundishwa shuleni nilikataa na ndipo nikaenda kuwaambia walimu wangu na mwisho wa siku nikaamua kutoroka"alisema Upendo
Kwa upande wake Nanyori (22) mkazi wa kata ya Musa ndani ya wilaya ya Arumeru mkoani Arusha naye pia alilazimika kukimbia nyumbani kutokana na kutaka kukeketwa na wazazi wake mara baada ya kumpatia mwanamme alietaka kumuona
"Mimi nilikuwa na soma kidato cha pili baba yangu akawa ameniambia niache shule kwani amenipatia bwana lakini pia aliniambia pia natakiwa nikeketwe kwanza ndipo niolewe maana mila na tamaduni zetu zinatutaka watoto kike tufanyiwe hivyo ,nilikataa na alinipiga sana na kuniambia lazima nifanyiwe tohara maana tayari alishachukuwa ng'ombe Kwa ajili ya mahari yangu na nilazima sio ombi
Mara baada ya mama kuona nalazimishwa na teari nilishakataa ndio mama akaamua kunisaidia na kunitorosha Ili nisifanyiwe kitendo hicho ,Mimi nilikataa kwakuwa teari nilishasikiaga madhara ya kukeketwa hivyo nilikuwa naogopa sana kufanyiwa kitendo hicho nilifurahia sana kusaidiwa na mama kutoroka na kuweza kunitafutia msaada wa kituo hichi kilichonipokea cha HIMD ambacho kinanisomesha vizuri
WATAALAMU WANASEMAJE KUHUSU UKEKETAJI?
Mkurugenzi wa HIMD Mackrine Ruman akiongea na mwandishi wa habari hizi
Mkurugenzi wa asasi isikuwa ya kiserikali inayowahifadhi mabinti waliokimbia majumbani kwao kutokanana kukimbia kufanyiwa ukeketaji pamoja na ndoa za utotoni HIMD, Mackrine Ruman aliieleza kuwa jamii ya wafugaji wa kimasai bado elimu ya mtoto wa kike inaendelea kukabiliwa na matatizo kutokana na baadhi ya mila na desturi ikiwemo ya tohara Kwa wanawake
Alibainisha vitendo hivyo vimetajwa kuchangiwa na kukosekana Kwa usawa wa kijinsia katika jamii hiyo huku mfumo dume ukiwa umetawala katika jamii hiyo licha ya kuwa jitihada nyingi zinafanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbambali kukabiliana na tatizo hili .
"Kwa Kushirikiana na viongozi wa vijiji kadhaa tumeweza kusaidia wanafunzi ambao wengi wao wanasoma darasa la saba waliokimbia kukeketwa na kuwapatia msaada wa elimu na makazi , kufuatia juhudi hizo tumeweza kuwasaidia wasichana zaidi ya 25 wa shule za msingi katika wilaya ya Monduli pamoja na longido kuepushwa na ukeketaji katika likizo iliosha swala ambalo ni hatua kubwa sana na juhudi kubwa sana tulizozifanya,na niseme tu tusingewasaidia wasichana hawa kuwatorosha ungekuta wote wamekeketwa Kwa nguvu ma hata wengine tungewapoteza"
Wanafunzi hao wa jamii ya kifugaji wa kabila la kimasai wamenusurika kufanyiwa ukeketaji baada ya kupelekwa kwenye nyumba salama ambayo ni maalimu kwa ajili ya waathirika na manusura wa vitendo vya ukeketaji wa kijinsia
Baadhi ya vifaa ambavyo mang'ariba wanavitumia kipindi wakikeketa wasichana hao
SHERIA YA SERIKALI INASEMAJE KUHUSIANA NA UKEKETAJI
Mifumo ya kisheria, Tanzania imejikita katika misingi ya sheria za Kiingereza;tathmini ya mahakama juu ya vitendo vya sheria tafsiri yake haijitoshelezi.Ingawaje Katiba yaTanzania (1977)1haijaweka wazi kumbukumbu za vitendo hatarishi dhidi ya ukeketaji wa wanawake, Ibara ya 9Inapendekeza kwamba ni jukumu la Taifa kuheshimu na kulinda haki za binadamu,Kutambua usawa wa haki za mwanamke na mwanaume na kuondoa aina yeyote ya ubaguzi.
Kifungu 13 kimeweka bayana usawa kinasema ‘watu wote wanahaki sawa na wapochini ya sheria’ na inadai Nchi kutekeleza taratibu kwa kuweka bayana kwambahamna mtu yeyote anatakiwa kupitia mateso, matendo yasiyo ya kibinadamu au vitendo vya kumdhalilisha mtu. ’Kifungu cha 16pia kinasema,' Kila mtu anastahili
heshima na kinga ya mtu wake 'na' faragha ya mtu wake '.
Sheria kuu inayohalalisha jinai nchini Tanzania ni Sheria ya Maalum ya Makosa ya Kijinsia 1998 (SOSPA), ambayo ilirekebisha Sehemu ya 169 ya Sheria ya Adhabu na inadhibiti ukeketaji kwa
wasichana chini ya miaka 18.2
Kwa kuongezea, Kifungu cha Sheria ya Mtoto 20094 Ibara 13(1)Ni kosa la jinai‘kumsababishia mtoto mateso , au adhabu za kikatili, matendo yasiyo ya kibidamu au vitendo vya kumdhalilisha ambavyo ni pamoja na mazoea ya tamaduni ambazo hazina utu au zinasababisha maumivu kimwili na kiakili kwa mtoto’
kama Sheria inayomlinda mtoto, Ibara 18inaruhusu pia mahakama kutoa amri ya huduma au amri ya huduma ya mda mfupi au kumuondoa mtoto kwenye hali
yeyoye hatarishi.
NINI KIFANYIKE KUONDOA UKEKETAJI NCHINI TANZANIA?
Kwa mujibu wa wadau wahasasi zisizokuwa za kiserikali HIMD wanasema kuwa ni vyema sheria iongeze adhabu za watu wote wanajiusisha na maswala ya keketa wasichana na mabinti
Elimu pia itolewe Kwa maghariba ambao bado wanafanya shughuli hizo za ukeketaji,elimu itolewe Kwa wazee wa Mila ,elimu itolewe Kwa wasichana pamoja nawanawake wa jamii ya kifugaji juu ya mathara yatokanayo na kitendo hicho.
Makala hii imeandikwa na kuandaliwa na Mwandishi wa habari Woinde Shizza wa Libeneke la kaskazini blog




0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia