ZAIDI WANANCHI LAKI MOJA MANISPAA YA IRINGA WAMEPATA CHANJO YA UVIKO-19

Mratibu msaidizi wa Chanjo manispaa ya Iringa Betha Lyimo akiongea na waandishi wa habari kutoa taarifa ya hali ya wananchi ambao wamepata chanjo ya UVIKO 19 Manispaa ya Iringa
Mratibu msaidizi wa Chanjo manispaa ya Iringa Betha Lyimo akiongea na waandishi wa habari kutoa taarifa ya hali ya wananchi ambao wamepata chanjo ya UVIKO 19 Manispaa ya Iringa

 
Na Fredy Mgunda,Iringa.

 

Zaidi ya wananchi laki moja halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa, wamepata chanjo ya ugonjwa wa UVIKO-19 sawa na asilimia 89 ya kuvuka lengo la serikali la kuchanja asilimia 70 hadi kufikia mwezi Desemba mwaka huu.

 

Akizugumza na wandishi wa habari wakati kutoa taarifa kwa umma kuhusu maendeleo ya chanjo ya Uviko-19 katika Halmshauri ya Manispaa ya Iringa Kaimu Mganga Mkuu Manispaa ya Iringa Dr Godfrey Mtunzi amesema kuwa hapo awali lengo lilikuwa ni kuchanja watu 123,418.

 

“Toka wameanza kutoa chanjo ya uviko 19 kwa wananchi manispaa ya iringa tumewafikia wananchi 110,135 sawa na asilimia 89 na kunapenda kuwamiza wananchi waendelee kupata chanjo ya uviko 19 kwa sababu ni salama kwa matumizi ya binadamu”, alisema Mtunzi

 

Kwa upande wake Dr. Clement Makoba Kutoka Hospitali ya Rufaa ya Iringa amesema kuwa ni vyema wananchi wakapata chanjo ya uviko 19 ili kukamilisha asilimia 11 zilizobaki na kufikia asilimia mia ya watu waliopata chanjo.

 

Amesema kuwa hawawezi kufanya majaribio kwa mwili watu kwa sababu chanjo hii ni salama hivyo serikali inasisitiza wananchi kuendelea kuchanja ili kuepusha kupoteza nguvu kazi ya Taifa.

 

 

Naye Mratibu msaidizi wa Chanjo manispaa ya Iringa Betha Lyimo alisema kuwa bado wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kuchanja.

 

“Tumeendelea kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo ya biashara maofisini, kwenye misikiti, makanisani na katika makundi mbalimbali kuhamasisha chanjo na toka wamepata chanjo hakuna madhara ambayo yameonekana kwa waliochanja” alisema Lymo.

 

 

Alisema kuwa wameendelea kutoa chanjo ya uviko 19 kupitia Mkoba ambao unalengo la kufika katika eneo ili kuwapatia chanjo wananchi ambao wanashindwa kufika katika vituo vya afya.

 

Baadhi ya Viongozi wa dini, Askofu Samuel shayo   na Katibu wa Kadhi Mkoa wa Iringa Ustaadh Abdallah Khalid Ndede wamesema kuwa wanashirikiana na waratibu wa afya ngazi ya jamii kuwahamasisha waumini wao kupata chanjo ya Uviko-19 kwa kuwa ni janga la kitaifa.

 

Walisema kuwa katika mafundisho ya Dini wameamrishwa kuwaelekeza waumini wao kuchukua tahadhari za kiafya endapo watakutana na majanga ya maradhi.

 

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia