Wakulima watakiwa kufanya uzalishaji wa vyakula bora utakao kidhi afya ya mwananchi
Afisa lishe mkoa wa Arusha Rose Mauya akiongea Kwa niaba ya mgeni rasmi ambaye ni afisa kilimo mkoa ,katika maathimisho ya siku ya chakula dunia ambayo Kwa mkoa wa Arusha wameathimisha actober 18 ndani ya viwanja vya shirika linalohusiana na utafiti wa mboga na matunda(world vegetables center)lililopo Tengeru ndani ya halmashauri ya Meru Mkoani ArushaBaadhi ya wananchi waliouthuria maathimisho hayo wakifuatilia uzinduzi
meneja wa kanda ya kati wa benki ya maendeleo ya kilimo (TADB) Voda's Mwanakatwe akiongea na waandishi wa habari
Na Woinde Shizza , ARUSHA
Wakulima wametakiwa kufanya uzalishaji wa vyakula bora wenye lishe bora utakao kidhi afya ya mwananchi baada ya uzalishaji.
Aidha pia wametakiwa kuzalisha chakula bora kitakacho kidhi afya ya binadamu ,pamoja na kujali zaidi ulaji wa mwananchi na sio kujali masoko tu.
Hayo yameelezwa na Rose Mauya afisa lishe mkoa wa Arusha wakati akiongea katika maathimisho ya siku ya chakula dunia ambayo kwa mkoa wa Arusha wameathimisha actober 18 ndani ya makao makuu ya shirika linalohusiana na utafiti wa mboga na matunda(world vegetables center)lililopo Tengeru ndani ya halmashauri ya Meru Mkoani Arusha ambapo aliwataka wakulima kufanya uzalishaji unaotosheleza pamoja na wenye kuleta chakula ambacho kina lishe na nutrition .
Alisema kuwa kumekuwa na uhaba wa chakula kwakuwa chakula kingi kinachozalishwa kimeelekezwa kwenye masoko tu ,wakati tunajua kwamba sikuzinavyozidi kwenda tuna ongezeka ,watoto wanakuwa na wengine wapo shuleni ,hivyo nivyema wakulima wanapo zalisha wakumbuke kurudi kwenye jadi zetu za kuzalisha vyakula kwa ajili ya biashara pamoja na vyakula vya familia zetu.
"Tunaona kwamba kunawimbi kubwa sasa, watoto wanapata shida katika lishe tujiulize wanapata shida kwanini? Kwa vile vyakula tunavizalisha ?lakini utumiaji au matumizi sahihi ya vyakula hawayafati hivyo tunawaambia wakulima wetu wanapo zalisha pia wazingatie matumizi sahihi ya vyakula ili vyakula hivyo vitumike kwa ajili ya kutuongezea kipato lakini pia katika ujengaji wa afya zetu ili ziweze kuimarika"alisema Rose
Aidha alifafanua kuwa hali ya lishe kwa mkoa wa Arusha inaendelea kuimarika kwani tatizo kubwa la udumavu lililokuwa linasumbua ,yaani la mtoto kukua kwa kuongezeka kwa umri lakini kimo akiongezeki limepungua kitaifa tupo kwa asilimia 32% lakini kimkoa wa Arusha tupo asilimia 25% na tunatumaini kwamba utafiti uliofanyika mwaka huu ukitoka utaonyesha hali hiyo imepungua zaidi.
Kwa upande wake meneja wa kanda ya kati wa benki ya maendeleo ya kilimo (TADB) Voda's Mwanakatwe alisema wao kama mdau sekta ya kilimo , walianzishwa na serikali kuhakikisha kwamba kunautoshelevu wa chakula,pamoja na kuhakikisha sekta ya kilimo inakuwa kutoka kwenye kilimo cha kujikimu kwenda kwenye kilimo cha biashara.
Alisema kuwa malengo ya kuanzishwa yakiwa ni kuhakikisha kwamba uzalishaji unaongezeka na unakuwa na tija pamoja na kuhakikisha kwamba kunakuwa na upungufu wa upotevu wa mazao baada ya mavuno ambapo ripoti zinaonyesha chakula kinapotea kati ya asilimia 10%hadi asilimia 30% .
"Moja ya maeneo ambayo tunahakikisha yanakuwa na tija ni kwenye uhifadhi wa chakula,pamoja na hilo pia tumekuwa tunahakikisha kwamba tunawekeza zaidi kwenye kuongeza dhamani kwenye mazao " alisema Mwanakatwe
Alitaja kauli mbiu ya maathimisho haya ya siku ya chakula duniani kuwa ni uzalishaji bora ,lishe bora ,mazingira bora na maisha bora kwa wote habaki mtu nyuma.



0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia