KADI YA NJANO SULUHISHO LA JUKWAA LA UBADILISHAJI MALI
Mtu
akikata bima ya kadi ya Njano ya mtu wa tatu inaruhusu kuweza kupita na gari
katika nchi zilizotuzunguka ikiwemo Zambia Malawi, Zimbabwe, Uganda Rwanda
,Burundi ,Msumbiji ,Jibuti , Sudani kusini na Sudan bila kusimamishwa na iwapo
atasababisha madhara yoyote kwa mtu wa tatu bima itagharamia gharama zote za
kumlipa
Naibu waziri wa fedha ,Hamad Chande amewataka watanzania
kutumia fursa ya bima ya kimataifa ya mtu wa tatu (Yellow Card) kama njia moja
wapo ya kukuza biashara na uchumi wa nchi na kuwarahisishia wafanyabiashara
wanaosafiri kibiashara nje ya nchi.
Chande ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa 36 wa baraza la
usimamizi wa bima ya mtu wa tatu NIC, unaokutanisha wanachama wa Soko la
pamoja la Mashariki na kusini mwa afrika (COMESA) na wasiowanachama
,unaofanyika kwa siku tatu jijini Arusha.
Aliwataka wananchi na wafanyabiashara kutumia yellow kadi halisi
na sio feki kama ilivyo kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakihujumu taifa kwa
kufumia kadi zisizosahihi.
Alifafanua kuwa faida ya yellow kadi unaweza kuitumia popote
katika nchi yoyote wanachama ili kukinga biashara au ajali ukiwa nje ya
nchi.
"Unapokata kadi ya Njano Tanzania unaweza kutumia kadi
ile ile nchi za jirani kwa thamani ile ile ulionunua katika nchi husika na hii
ni faida kubwa kibiashara kwa wafanyabiashara wanaochukua ama kupeleka bidhaa
nje ya nchi"alisema
Alisisitiza kuwa unapokuwa na kadi ya njano ni kinga kwa biashara
hasa pale kunapotokea dharura ya ajali ya gari au ya moto katika biashara
kunakufanya usisononoke kwa kuwa bima hiyo itakulipa fidia mali zako.
Aliitaka baraza la msimamizi wa bima ya mtu wa tatu (yellow
kadi)kulipa fidia kwa waathirika wakati ndani ya simu 30 ili mtu awe na imani
na mashirika ya bima.
Awali mkurugenzi mtendaji shirika la bima nchini NIC dkt Rehema
Dorie alisema kuwa mkutano huo unakutanisha nchi wanachama wa soko la pamoja la
mashariki na kusini mwa afrika (COMESA) na wasio wanachama zinazofanyabiashara
ya bima ya mtu wa tatu.
Dkt Dolie ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la usimamizi wa bima
ya mtu wa tatu kwa nchi za COMESA alisema yellow kadi inampa kinga na
kumrahisishia mfanyabiashara anayesafiri ama kusafirisha mizigo katika nchi za
comesa bila hofu ukizingatia kwamba Tanzania ni kitovu cha biashara kwa
kuwa inabandari kubwa zinazopokea mizigo .
" hii inalipa mara moja kutokana na sheria za nchi
husika bila kujali gharama zilizopo".
Dkt Dolie ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la usimamizi wa bima
ya mtu wa tatu kwa nchi za COMESA alisema yellow kadi inampa kinga na
kumrahisishia mfanyabiashara anayesafiri ama kusafirisha mizigo katika nchi za
comesa bila hofu
habari hii imeandikwa na mwandishi Woinde Shizza,Arusha

0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia