FAHAMU CHANGAMOTO ZINAZO WAKUTA WANAWAKE SOKONI

Sokoni  ni kati ya maeneo ambayo wanawake wamekuwa wakifanyiwa ukatili ikiwamo kutukanwa, kupewa majibu ya kejeli, wenye maumbile makubwa kushikwashikwa, kuchekwa, kucharuliwa na kudharauliwa



Unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsia ni kati ya changamoto zinazochangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma jitihada za wanawake katika kujikwamua kiuchumi.

Sokoni ni kati ya maeneo ambayo wanawake wamekuwa wakifanyiwa ukatili ikiwamo kutukanwa, kupewa majibu ya kejeli, wenye maumbile makubwa kushikwashikwa, kuchekwa, kucharuliwa na kudharauliwa.


Licha ya jitihada zinazofanywa na wanawake kujikomboa kiuchumi bado wanakumbana na unyanyasaji na udhalilishaji katika maeneo yao ya biasharaWapo baadhi ya wanawake waliokata tamaa na kuachana na shughuli hiyo kwa kuogopa karaha lakini wapo, walioamua kupambana bila kujali chochote.


Kwa mujibu wa Taasisi ya ‘Equality for Growth (EfG)’ asilimia 90 ya wanawake wafanyao kazi katika masoko nchini Tanzania wanakumbana na unyanyasaji, ikiwamo lugha za matus


Simulizi za wanawake soko


Mmoja wa wanawake waliowahi kukumbana na ukatili huo katika Soko la Kariakoo, jijini Dar es Salaam, Hellen Tuniya anasema haikuwa rahisi kuvumilia lugha za kejeli aliyopewa baada ya kushindwa kurejesha chenji kwa mteja wake sokoni hapo


“Kuna mteja aliwahi kunijibu vibaya kiasi cha kunitoa machozi, alisema ‘mwanamke ukawe wewe! Ona ulivyopauka, sura kama vitunguu unavyouza’, nilitetemeka, nikataka kumpiga ila nikaamua kuachana naye,” anasem


Wanawake wenye maumbile makubwa hasa ‘makalio’ hukutana na changamoto kubwa ikiwa kuitwa majina ya kejeli ukatili wa aina yake ikiwamo kuitwa majina yenye sifa mbaya kwenye jamii kama kejeli kama ‘chura’, na mengine meng


Wanawake wengi waliozungumza na Mwananchi kila mmoja alikuwa na kero yake anayodai kuwa, inasababisha kurudisha nyuma jitihada zake za kupambana na ugumu wa maisha.


Licha ya wengi kulalamikia hali ngumu ya uchumi, wanasema mitaji midogo na masharti magumu ya mikopo toka taasisi za kifedha.


Mfanyabiashara wa Soko la Buguruni, Ester Lupia anasema anaamini kitendo cha kutoamini na kukosa dhamana kwa sababu ya biashara yake ya mali mbichi anayoifanya ni ukatili.


“Binafsi sijatukanwa ila kuna maeneo mengi nimeenda kukopa walikaa kunipa hela, walisema ni mwanamke halafu biashara yangu inaweza kufa wakati wowote. Tunaomba Serikali itusaidie, tudhaminiwe,” anasema.


Lupia na wanawake wengi wanasema licha ya kuwa wamejiunga kwenye vikundi vya uchumi hawajaweza kupata mikopo jambo ambalo, linaendelea kuwatesa.


Halima Juma, aliyewahi kufanya biashara kwenye Soko la Mabibo anasema ukatili aliowahi kufanyiwa na kuwa hatausahau ni siku aliposhikwa makalio na kuimbiwa wimbo wa chura.


“Nilijiona kama sijavaa nguo na tangu siku hiyo sitaki tena kuuza sokoni. Nimefungua genge nyumbani,” anasema.


Mwenyekiti wa EfG, Mussa Mlawa anasema walifanya utafiti huo baada ya kupata malalamiko mengi ya kuwapo kwa manyanyaso toka kwa wanawake wanaofanya biashara sokoni.


Anasema baada ya matokeo hayo wakalazimika kuanzisha elimu maalumu na kuwataka wanawake na wadau sokoni kushirikiana katika ulinzi wa haki za wanawake.


Matokeo ya utafiti


Katika utafiti huo, ilionekana kuwa wanawake wafanyabiashara wa sokoni ni kwa nadra sana wameshirikishwa katika kufanya maamuzi na kuingizwa katika kamati za masoko.


Utafiti huo unaonyesha kuwa kati ya viongozi 89 wa kamati za masoko, wanawake walikuwa ni 14 tu.


Pia mikakati ngingine ya EFG ni kuanzishwa kwa vikundi vya wanawake vinavyosimamiwa na wanawake wenyewe na kutolewa mafunzo ya uongozi.


Anaitaja mikakati mingine kuwa ni kuendeshwa kwa mafunzo ya mbinu za utetezi na ushawishi kwa wanawake, kujenga uelewa wa viongozi wa soko juu masuala ya jinsi na jinsia na uhusiano wake na masoko, kuanzishwa kwa vikundi vya ufuatiliaji wa mapato na matumizi vya wafanyabiashara ndani ya soko pamoja na kuwaunganisha wanawake na watunga sera na viongozi wa kitaifa.


Mafanikio


Taasisi hiyo inasema tayari wameanza kupata mafanikio tangu waanze utekelezaji wa kazi kwenye masoko ikiwamo wanawake wenyewe kujitambua na kujua nafasi yao katika kuchangia uchumi.


Mafanikio mengine yanayotajwa kwenye teerifa ya utekelezaji wa kazi hivyo kuwa ni kuanzishwa kwa Vikundi vya umoja wa wanawake kuanzishwa katika masoko 41 ya mikoa tisa ya Tanzania bara vyenye jumla ya wanachama zaidi ya 6,500.





Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post