Wanawake watakiwa kuelewa matumizi sahihi ya mitandao ili kuepuka ukatili wa kijinsia

 


Mkurugenzi wa Zaina Foundation Zaituni Njovu amewataka waandishi wa habari kuwahamasisha wananchi namna bora ya matumizi ya mitandao ili kuepukana na ukatili wa kijinsia.




Ameyasema hayo katika mafunzo ya kuelimisha waandishi juu ya matumizi sahihi ya mitandao yalioandaliwa na zaina foundation huko hotel ya verde Mtoni Wilaya ya Magharib "A" Unguja alisema tumewapatia elimu waandishi wa habari juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii lengo ni kuwaelimisha jamii ili kupunguza changamoto za ukatili ya kinjisia ambao unafanyika mitandaoni kwa njia tofauti.




"Alisema watu hutumia mitandao kufanya udhalilishaji kwa wanawake kuweza kutuma picha na maelezo ambazo zinaweza kuwa kweli au sio za kweli kwa lengo tu la kumchafua heshima mtu jambo ambalo husababisha msongo wa mawazo, kashfa, kunyanyapaliwa na jamii, na hata kujiuwa"




Aidha alisihi wanahabari kufahamisha jamii kuachana na tabia ya kueka picha za watoto wao mitandaoni kwani zinaweza kutumiwa vibaya na kuongezeka ukatili wa kijinsia.




Unapoeka picha ya mtoto mtandaoni ina kuwa ni hatari kwa sababu mtu yoyote anaweza kutumia sura hiyo kwa malengo tofauti yenye dhamira mbaya.




Alisema kwa mujibu wa utafiti walizofanya zinaonesha kuwa asilimia 51%ya watoto wameshadhalilishwa na 85% kufanyiwa unyanyasaji yote hayo yametokea baada wazazi kutuma picha za watoto wao kwenye mitandao. 




Pia aliwataka wanajamii kuacha kijirekodi picha chafu wakiwa katika mahusiano kwani baada ya uhusiano kuvunjika huzituma mitandaoni na kusababisha taharuki kwa jamii pamoja na familia.




Nae Afisa Program kutoka zaina foundation Dorina Mathayo aliwasisitiza waandishi kutumia password mazubuti ambayo itakuwa vigumu wengine kuielewa ili kujihakikishia usalama wa kazi zako.




"alisema password lazima ichanganye nambar, maneno na maneno maalumu ili watu wasijuwe kwa urahisi"




Aidha aliwataka waandishi kuepuka kubadilishana password pamoja na vifaa vya kazi ili kuweza kujilinda na kuweka usalama wa mambo yao hasa kwa kipindi hichi kinachoelekea uchaguzi.




Kitu cha kwanza unatakiwa uwe na password tofauti tofauti na iwe siri yako usibadilishane na hata watu wa karibu kwani kufanya hivyo kutasaidia watu kujilinda zaidi.




Pia aliwasihi kuweza kuwa makini na maongezi yanayoongea na ujumbe wanazotuma katika simu kwasababu mitandao ina kawaida ya kuhifadhi kumbukumbu za vitu inaweza kukupatia shida bila ya kutarajia.


Kwa upande wao waandishi wa habari mwanaisha bakari wa Zbc na kazija Mwinyi wa asalamu fm wamesema ni vizuri kupatiwa mafunzo hayo kwani wameweza kuelewa namna ya kujilinda na vipi unaweza kumkatili mtu kijinsia pamoja na kutobadilishana vifaa vya kazi ili kujihakikishia usalama 

 

Aidha waliwaomba zaina foundation licha ya kuwapa wao jukumu la kuelimisha jamii lakini na wao waweze kufanya mafunzo hayo kwenye maeneo mbali mbali hapa nchini ili kushirikiana kwa pamoja kusambza elimu hiyo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post