WANANCHI 291 WAKIWA NA MIFUGO 686 WASEMA "BYE BYE" NGORONGORO

 


Kundi la 17 katika awamu ya pili lenye kaya 47, watu 291 na mifugo 686 limehama kwa hiari kutoka hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera, Handeni Tanga pamoja na maeneo mengine waliyochagua.

 


Kati ya kaya hizo 47, kaya 41 zenye watu 256 na mifugo 525 zimeelekea kijiji cha Msomera na kaya 6 zenye watu 35 na mifugo 161 zimeelekea maeneo mengine ikiwemo Meatu, Simiyu na Simanjiro mkoani Manyara.


Kwa mujibu wa Afisa Uhifadhi Mkuu Flora Assey ambae ni Meneja mradi wa kuhamisha wananchi wanaojiandikisha kuhama kwa hiyari ndani ya hifadhi, tangu zoezi hilo lilipoanza mwezi Juni, 2022 hadi kufikia tarehe 15 Juni, 2024 jumla ya kaya 1,519 zenye watu 9,251 na mifugo 38,784 zimeshahama ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kwenda kijiji cha Msomera na maeneo mengine.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post