Katika dunia ya sasa yenye teknolojia ya hali ya juu, usalama wa mtandao umekuwa suala nyeti sana, Samwel alikuwa mfanyakazi hodari katika kampuni ya teknolojia ,Siku moja alipokea barua pepe iliyoonekana kama kutoka kwa mteja muhimu, ikimtaka afungue kiunganishi kilichokuwa kimeambatanishwa.,Bila kusita, Samwel alifungua kiunganishi hicho akidhani ni kazi ya kawaida.
Dakika chache baadaye, aligundua kuwa kompyuta yake ilianza kufanya kazi kwa njia isiyo ya kawaida, Programu za kampuni ziliacha kufanya kazi na taarifa muhimu zilianza kupotea ,Samwel alikuwa amedukuliwa! Hili lilisababisha hasara kubwa kwa kampuni na ilichukua muda kurejesha mfumo wa usalama.
Kutokana na tukio hilo, kampuni iliamua kutoa mafunzo ya kina kwa wafanyakazi wake juu ya usalama wa mtandao.
Waliwahimiza kuepuka kufungua viunganishi au kupakua viambatisho kutoka kwa vyanzo visivyojulikana, kwani ni njia mojawapo ya kuzuia mashambulizi ya kimtandao.
Hatua hizi zilisaidia sana katika kuboresha usalama wa kampuni na kuzuia tukio kama hilo kutokea tena.
Ni muhimu sana kuwa makini na viunganishi na viambatisho tunavyopokea mtandaoni ili kulinda taarifa zetu na mifumo yetu.