BENKI YA BARODA YATOA MSAADA KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA ARUSHA

 

Mkurugenzi wa benki ya Baroda wa tatu kushoto  S.K Palanivell  pamoja na wafanyakazi wengine wa benki hiyo wakiwagawia watoto  wa kituo cha yatima E.venerate Orphanage zawadi kipindi walipowatembelea

Na Woinde Shizza ,Arusha 

Benki ya Baroda imetoa msaada wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2 katika kituo cha kulelea watoto yatima cha E. Venerate Orphanage kilichopo Kwamrefu, Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Msaada huo ulijumuisha sukari, mafuta ya kupikia, mchele, maharage, unga, chumvi, sabuni pamoja na magodoro kwa ajili ya watoto wanaolelewa kituoni hapo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa benki hiyo, S.K Palanivell, alisema mchango huo ni sehemu ya mkakati wa benki kurudisha kwa jamii kupitia shughuli za kijamii.

Meneja wa benki hiyo tawi la Arusha, Gabinus Pole Pole akikabidhi msimamizi wa kituo Sophia Maliaki moja ya magodoro waliyowapelekea 

“Tunatambua changamoto zinazokabili makundi yenye uhitaji, hivyo tumeona tuungane kuwafariji watoto hawa kwa mchango huu, Vifaa hivi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2 ni ishara ya upendo wetu kwa jamii. 

alisema benki ya Boroda haitajikita tu katika huduma za kifedha, bali pia inataka kuwa mshirika wa karibu wa jamii, Constriction tunaposhirikiana sote tunaweza kubadilisha maisha ya watoto hawa na kuwapa matumaini mapya,” alisema Palanivell.

Kwa upande wake, Meneja wa benki hiyo tawi la Arusha, Gabinus Pole Pole, alisema benki hiyo imekuwa na utaratibu wa kusaidia jamii kwa nyanja mbalimbali ikiwemo shule kwa kuchangia madawati, hospitali pamoja na makundi yenye uhitaji.

 “Jamii ndio msingi wa kila taasisi ,Ndiyo maana tumejikita kushirikiana na wananchi kwa vitendo ,leo tumewakumbuka watoto yatima, kesho tunaweza kuwasaidia wagonjwa hospitalini au wanafunzi mashuleni ,tunataka jamii ijue kwamba Baroda ipo karibu nao, kwa kuwa maendeleo ya jamii ndiyo msingi wa mafanikio ya taasisi yetu,” alisema Pole Pole.



Aidha, Msimamizi wa kituo hicho, Sophia Maliaki, alisema kituo hicho kinahudumia watoto wapatao 67 wakiwemo yatima na waliotelekezwa na wazazi, ambapo baadhi wamepata wafadhili na wengine husoma shule za kawaida.

Alifafanua kuwa changamoto kubwa zinazowakabili ni ukosefu wa chakula, nguo na umeme wa kuwawashia watoto nyakati za kusoma.

 “Kwa kweli suala la chakula limekuwa changamoto kubwa sana Lakini changamoto nyingine ni watoto kukosa nguo za kuvaa na pia kukaa gizani nyakati za kusoma kutokana na ukosefu wa umeme ,Wadau wakijitokeza, tungeweza kuwajengea mazingira bora ya kusoma na kuishi,” alisema Maliaki.

Maliaki aliomba pia wananchi wa kawaida kujitokeza na kuchangia nguo kwa watoto hao, akisema hata msaada mdogo unaweza kuleta tofauti kubwa katika maisha yao.

“Watoto wetu wanakabiliwa pia na changamoto ya ukosefu wa nguo ,Hata kama mtu hana chakula cha kuchangia, anaweza kuleta nguo ambazo hazitumiki majumbani ,hilo litawasaidia watoto wetu kuishi kwa heshima na furaha kama watoto wengine tunawaomba wananchi, mashirika na taasisi mbalimbali kutuunga mkono ,Mungu atawabariki kwa moyo wenu wa upendo,” alisisitiza Maliaki.

Kwa kumalizia, Maliaki aliishukuru benki hiyo

 “Tunashukuru sana Benki ya Baroda kwa msaada mkubwa wa thamani ya zaidi ya milioni mbili ,Mmetuletea faraja kubwa na tumaini jipya kwa watoto wetu,tunaomba pia muendelee kutukumbuka kwa siku zijazo, kwani changamoto zetu bado ni nyingi,” alisema kwa hisia.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia