TASAC-YATAKA KAMPUNI BINAFSI KUTOJIHUSISHA UONDOSHAJI WA KEMIKALI NA VILIPUZI MIGODINI
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA
la Uwakala wa Meli Tanzania ( TASAC ), limewataka wachimbaji wadogo na
wakubwa wa madini pamoja na Kampuni za ugomboaji na uondoshaji wa
shehena kuhakikisha kemikali na vilipuzi vinavyotumika kwenye migodi
zinaondolewa na wataalam wa TASAC pekee na si vinginevyo.
Hayo
alibanisha Mkurugenzi wa Huduma za Shirika hilo Hamid Mbegu kwenye
Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini, yanayofanyika
Mkoani Geita.
Amesema
kuwa kisheria TASAC ndiyo Taasisi pekee ya Serikali imepewa jukumu la
kipekee la kusimamia masuala yote yanayohusiana na ugomboaji na
uondoshaji wa shehena za vilipuzi kama baruti na kemikali zinazotumika
katika shughuli za uchimbaji na usafishaji wa madini nchini kwa mujibu
wa Sheria ya Uwakala wa Meli, Kifungu Na.7, Sura 415.
"Baadhi
ya shehena hizi ni sumu na zenye madhara makubwa, hivyo Serikali
kupitia TASAC,inapaswa kusimamia kikamilifu uondoshaji wake. Rai yetu
kwa wachimbaji, makampuni ya uagizaji na ya ugomboaji na uondoshaji ni
kutambua kwamba jukumu la kuondoa shehena hizi ni la TASAC pekee,
wanaopitisha shehena kupitia kampuni binafsi wanakiuka sheria, "
amesisitiza.
Mbegu
amesema kumekuwepo na baadhi ya kampuni ambazo zimekuwa zikisafirisha
kemikali hatarishi kama Sodium Cynite, kupitia kampuni binafsi kwa ajili
ya shughuli za ulipuaji migodini, jambo ambalo linaelezwa kuwa ni
kinyume cha sheria na taratibu







0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia