MAHAFALI YA ARUSHA ALLIANCE YAWA CHACHU YA WAZAZI KUSUKUMA ELIMU YA WATOTO
Na Woinde Shizza, Arusha
Arusha Alliance School imefanya hafla ya mahafali ya 16 ya darasa la saba , ambapo jumla ya wanafunzi 141 walihitimu mwaka wa masomo, ikionyesha mafanikio makubwa ya shule katika kutoa elimu bora inayokidhi mahitaji ya wakati na kuendeleza maadili mema kwa watoto.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Shule hiyo Magdalena Mapongo aliweka mkazo mkubwa kwenye umuhimu wa elimu yenye msingi wa maadili, huku akiahidi kuendelea kutoa fursa kwa wanafunzi kuwa mabalozi wa jamii na kuendeleza maarifa waliyopewa.
“Shule yetu inalenga kutoa elimu ya kisasa inayozingatia maadili mema, Watoto wanapokuwa watu wa faida wa kutegemewa na taifa pamoja na familia zao, tutaona matokeo halisi ya elimu bora,” alisema.
Mkuu huyo wa Shule alibainisha kuwa shule hiyo ilianzishwa mwaka 2007 ikiwa na wanafunzi 18 tu, lakini sasa ivi idadi imeongezeka mara dufu na jumla ya wanafunzi 116 walihitimu darasa la Saba na kukubainisha kuwa wanafunzi wote wanatarajiwa kufaulu vizuri kutokana na mafunzo na maadili wanayopata huku Alisisitiza kuwa Shule hiyo imeendelea kuongoza kwa kutoa elimu bora pamoja na malezi mema kwa watoto.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na mkaguzi WA polisi na mkuu wa dawati la jinsia na watoto kituo cha polisi Muriet Wilson Maatogoro, ambaye alikuwa mgeni rasmi Alitumia fursa hiyo kuagiza watoto wasome Methali 22, akisisitiza umuhimu wa kuepuka tabia zisizo za faida zinazoweza kupumbaza akili zao na kuwataka kuendeleza maarifa waliyopewa shuleni.
“Watoto mnapaswa kutumia maarifa mliyopata shuleni kuwa watu wa faida na wa kuaminika, Methali 22 ni nyenzo muhimu ya mafunzo ya maisha, na kila mtoto anapaswa kuisoma na kuitumia,” alisema Kamanda huyo, huku akisisitiza pia ushirikiano kati ya shule, wazazi, na polisi katika malezi na usalama wa watoto.
Aidha wanafunzi walisisitiziwa umuhimu wa kuendeleza maarifa waliyopewa shuleni, huku wakisisitiza kuwa mahafali haya yanapaswa kuwa chachu ya wazazi kuendelea kupeleka watoto wao shuleni ili wapate elimu bora na maadili mema.
Aidha, wazazi walihimizwa kushirikiana kwa karibu na shule katika malezi ya watoto, kuhakikisha kizazi kijacho kimelelewa kwa maadili mema na maarifa ya kisasa ambapo wamesisitiza kuwa makini katika kuhakikisha watoto wanakuwa salama na wanapata elimu bora.
“Tujumuike kujenga kizazi kizuri, tukishirikiana wazazi, walimu, na polisi kama njia ya kuhakikisha watoto wanakuwa watu wa faida kwa familia zao na taifa kwa ujumla"alisema




0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia