GOLGOTHA PRE & PRIMARY YASHEREKEA MIAKA 10, YAFANYA MAHAFALI YA 10 YA DARASA LA SABA



Na Mwandishi Wetu, Arusha

Shule ya Golgotha Pre & Primary School, iliyopo jijini Arusha, imeadhimisha kumbukizi ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake sambamba na kufanya mahafali ya 10 ya darasa la saba, hafla iliyohudhuriwa na wazazi, walezi na wageni waalikwa. Tukio hilo limeacha alama kubwa ya mafanikio katika sekta ya elimu ya awali na msingi.

Akizungumza katika sherehe hizo, Mkurugenzi wa shule hiyo, Vicky Kuga, alisema jumla ya wanafunzi 45 wamehitimu masomo yao mwaka huu na kueleza kuwa kwa kipindi chote cha miaka 10 shule hiyo imekuwa chachu ya kutoa elimu bora inayowaandaa wanafunzi kwa maisha ya baadae.

“Kila mwaka tunajivunia matokeo mazuri ya wanafunzi wetu Tunawalea kwa elimu ya kitaaluma, malezi ya kidini na pia mafunzo ya maadili mema ambayo yanawajenga kuwa raia wema kwa familia zao na taifa kwa ujumla,” alisema Kuga huku akipongeza walimu kwa mchango wao mkubwa.

Aliongeza kuwa shule hiyo imekuwa na utamaduni wa kufaulisha kwa viwango vya juu na tayari imezalisha wahitimu wengi ambao wanaendelea na masomo katika shule mbalimbali za sekondari wakifanya vyema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mwenza wa shule hiyo, Elias Kuga, alisema shule hiyo bado inatoa nafasi kwa wanafunzi wapya kuanzia elimu ya awali hadi darasa la saba, na kusisitiza kuwa ada inayotozwa ni nafuu hivyo wazazi wasisite kupeleka watoto wao.

Tunawaalika wazazi wote kujiunga nasi kwa sababu tuna mazingira bora ya kujifunzia, walimu wenye weledi na ada zetu ni nafuu Lengo letu ni kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora bila kikwazo cha gharama,” alisema Kuga.

Aidha, alibainisha kuwa shule hiyo imewekeza katika miundombinu ya kisasa ikiwemo madarasa yenye vifaa vya kisasa, maktaba na maeneo ya michezo ili kuhakikisha mtoto analelewa kimwili, kiakili na kimaadili.

Wazazi waliohudhuria sherehe hizo waliipongeza shule ya Golgotha kwa jitihada kubwa za kutoa elimu bora na malezi mema Walieleza kuwa shule hiyo imekuwa mfano wa kuigwa kutokana na nidhamu, usafi na usimamizi mzuri wa walimu na viongozi wake.






Sherehe hizo pia zilihusisha burudani mbalimbali ikiwemo nyimbo, ngoma na michezo iliyooneshwa na wanafunzi wa shule hiyo, hali iliyofanya tukio hilo kuwa la kipekee na la kukumbukwa.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia