BREAKING NEWS!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

MGOMBEA udiwani wa Kata ya Mjini Kati, Simba Seif (Chadema), amelazwa Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru akiwa mahututi baada ya kunyongwa na mahabusu wenzake akiwa kuwekwa ‘lock up’.



Kabla ya kunyongwa, Seif alifikishwa katika Mahakama ya Mkoa jana mchana kwa kile kilichodaiwa na wakala wa kampuni inashughulikia kukusanya ushuru wa kuegesha magari stendi ya mabasi yaendayo mikoani mjini hapa, kwa kuhoji kwanini kampuni hiyo ilikuwa ikikusanya ushuru hadi sikukuu ya Idd el Fitri.



Baada ya kukamatwa na polisi siku ya Idd, Seif alipewa dhamana na Mwenyekiti wa Wilaya wa Chadema, Derick Magomba hadi jana alipopigiwa simu na polisi wakimtaka kwenda mahakamani kujibu shtaka lake.



Kabla ya kesi yake kuanza, Seif alipelekwa mahabusu ya mahakamani hapo na ilidaiwa kuwa askari aliyekuwepo mlangani alimtaka ampe Sh. 20,000 ili asiingizwe ndani.



Aliposema kwamba hana hela, askari huyo alimwingiza ndani na hapo mahabusi waliokuwa ndani walimlaki kwa kumshambulia na kumnyonga.



Akizungumza kwa shida katika wodi ya wagonjwa mahututi, Seif alisema wakati akishambuliwa na wenzake, huku akipiga kelele za kuomba msaada, alisikia sauti ya askari aliyepo nje ikimweleza kuwa apigane kama anavyosimama kwenye majukwaa kuhutubia.



“Pigana kiume kama unavyosimama kwenye majukwaa kuhutubia,” Seif alijaribu kumnukuu askari huyo.



Hata hivyo, kadiri kelele zilivyozidi, watu waliokuwa nje ya mahabusu walimshinikiza askari huyo amfungue mlango ili kumwokoa.



Lakini ilidaiwa kuwa askari huyo aliwaeleza watu hao kuwa hawawezi kumfanya lolote na anaweza kuwapiga bastola na angewasingizia kwamba mahabusu walitaka kukimbia.



Hata hivyo, ilielezwa kuwa watu hao waliendelea kupiga kelele na wakaenda kumweleza hakimu ambaye alikuwa kesi hiyo ilikuwa mbele yake.



Alieleza kuwa hakimu alimwamuru askari huyo kufungua mlango na ndipo walipomkuta Seifi akiwa mahututi.



Baada ya hapo alikimbizwa hospitali ya Mount Meru kwa matibabu.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia