VIONGOZI WA AFC WAJIUZULU AKIWEMO KOCHA MKUUU

Viongozi kadhaa wa timu ya soka ya AFC ya mjini Arusha wameamua kujiuzulu kufuatia matokeo mabaya ya timu hiyo .

Mbali ya viongozi hao pia Kocha Mkuu wa timu ya AFC,Willfred Kidau naye umebwaga ‘’manyanga ‘’ kuelendelea kuifundisha timu hiyo.

Katika kamati hiyo iliyojiuzulu imeeleza kuwa itakabidhi taarifa kwa wanachama wa AFC katika mkutano siku jumapili.

Viongozi waliojiuzulu ni pamoja na katibu mkuu James Rugangira na msaidizi wake John Mhala wengine ni pamoja na mweka hazina Stone Mwabamba na msaidizi wake Joseph Joseph.

Wengine ni pamoja na John Mashaka na Charles Charles na Abas Utanga,viongozi wengine ambao bado hawajatoa msimamo wao ni pamoja na Mwenyekiti Peter Temu na mjumbe na timu meneja mkuu wa AFC Denis Shemtoi.

Taarifa ya jumla iliyosainiwa na katibu Msaidizi wa muda Mhala ilisema kuwa sababu kubwa ya kujiuzulu ni kushindwa kuwajibika ipasavyo kufuatia matokeo mabaya ya michezo mitano ya timu ya AFC.

Taarifa hiyo ilisema uongozi huo wa muda umeona kuwa hautakuwa tayari kuendelea kuiongoza timu hiyo kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume na matarajio yao na watashindwa kujieleza mbele ya wanachama .

‘’Tumeshindwa kuwajibika,tumeamua kujiuzulu ili wanachama wengine wenye uwezo wa kuongoza timu ili iweze kuiongoza timu hiyo’ilisema taarifa hiyo

Taarifa hiyo ilisema kuwa timu ya AFC iko katika hali nzuri kwani inalipwa mishahara,posho za safari na inakula bure kambini lakini inashindwa kuonyesha uwezo wa kisoka uwanjani hivyo labda labda uongozi wa muda ndio unachangia timu kufanya vibaya hivyo si busara kuendelea kung'ang'ania kuiongoza.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia