VIJANA wanaosadikiwa kuwa ni wa chama cha Tanzania Labour(TLP) wanadaiwa kufanya vurugu na kumjeruhi mfuasi wa chama cha mapinduzi aliyefahamika kwa jina la Makale Joseph mkazi wa Himo.

Tukio hilo limetokea Septemba 22 majira ya saa 6 mchana wakati mgombea Ubunge katika jimbo la Vunjo kwa tiketi ya TLP Agustino Mrema alipokuwa na wafuasi wake katika eneo la njia Panda akizundua Tawi la chama chake.

Akizungumza katika Zahanati ya Koggy iliyopo mji mdogo wa Himo ambako majeruhi alitibiwa,Mwenyekiti wa kijiji cha Himo Hussein Jamal alisema tukio hilo limetokea muda mchache baada ya Joseph kutelemka kwenye gari akiwa ameshika skafu ya CCM.

“Huyu bwana alikuwa akitokea kwenye shughuli zake ,alipofika njia panda akatelemka kwenye gari akiwa ameshikilia kitambaa cha CCM ,kumbe Mrema alikuwa katika eneo lile akizindua tawi ,ndipo vijana wake wakaanza kumshambulia.”alisema Jamal.

Alisema Mrema amekuwa akifanya mikutano mahala popote kwenye mikusanyiko ya watu bila kufuata utaratibu wa ratiba ambako hakuna ulinzi wa askari na kwamba vijana wake wamekuwa wakifanya vurugu pindi wanapokutana na wafuasi wa chama cha mapinduzi.

Akisimulia jinsi alivyovamiwa na wafuasi hao, Makala alisema baada ya kutelemka alianza kujifuta vumbi na kitambaa cha CCM,ndipo vijana hao wakamvamia na kuanza kumnyang’anya .

“Walikuja vijana zaidi ya 8 wakanivamia na kutaka kunipora kitambaa baada ya kukataa wakaanza kunipiga ndio matokeo yake wameniumiza kichwani nimeshonwa nyuzi 3”alisema Makala akiongeza kuwa katika vurugu hizo aliporwa simu na fedha kiasi cha shilingi 40,000 .

Mkuu wa wilaya ya Moshi Musa Samizi ambaye ni mlinzi wa amani alifika katika zahanati hiyo kumuona majeruhi hata hivyo hakuwa tayari kuzungumza chochote kwa madai suala hilo tayari limepelkwa kwenye vyombo vya sheria.

Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Lucas Ng’hoboko alisema hana taarifa za tukio hilo na kwamba matukio

Vurugu za mara kwa mara zimekuwa zikiripotiwa katika jimbo la Vunjo ambapo hivi karibuni wafuasi wa vyama vya CCM na TLP kwenye mji huo walichapana makonde baada ya kuzuka kwa mvutano baina yao saa chache kabla ya mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete kuwasili eneo hilo.

Vurugu hizo zilitokea baada ya wafuasi wa mgombea ubunge Jimbo la Vunjo, Augustino Mrema kupandisha bango kubwa linalomnadi katika lango la kuingilia mjini humo, ambapo wafuasi wa CCM waliwazuia na kuwalazimisha kulishusha.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia