Picha wa kwanza alivaa tisheti ya familia kondom ni meneja wa kanda ya kaskazini wa kampuni ya PSI Robison Kature akifuatiwa mganga mkuu wa halmashauri ya jiji ya Arusha Dr.Ibrahimu Isaack akimkabithi bi Edina Molel box la kondom katika kituo cha Ushauri nasaha cha kwa babu
Jumla ya kondom Elfu sabini na mbili zenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano na sabini zimegaiwa kwa wananchi wa naoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi katika kituo cha ushauri nasaha cha Padri Babu kilichopo mkoani hapa ili kuweza kusaidi kupunguza ongezeko la maambukizi ya virusi hivyo .
Msaada huo ambao umetolewa na shirika la PSI Tanzania imevishirikisha jumla ya vikundi 26 vya watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi jijini hapa.
Akikabidhi msaada huo meneja wa kampuni ya Psi mkoa wa Arusha na Manyara Christopher Mbajo amesema kuwa kampuni yao imeamua kutoa msaada huo wa kondom kutokana na maombi ambayo wameyapata kutoka kwa watu hao ambao wanaishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Alisema kuwa msaada huu wa kondom pia utasaidi kwa kiasi kikubwa kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi haswa kwa wale watu ambao hawaja athirika na pia wameona ni vyema kuwapa kwa sababu wao wenye wamekaa wakaona njia pekee ya wao kutoendelea kuneza virusi hivi vya ukimwi ni kutumia kondom.
"watu hawa ambao wanaishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi walikuja ofisini kwetu kutuomba tuwasaidie kondom ili waweze kutumia na kutoa elimu kwa wenzao watumie ili wasiweze kuendelea kupata maambukizo zaidi ya virusi hivi"alisema Mbajo.
Alibainisha kuwa mbali na hivyo kwa kitendo hichi cha kuwapatia msaada huu wa kondom kwa mara ya kwanza itawajengea tabia ya kutumia kondom hata kama hizi zitaisha watenda kununu pia watawashauri watu wengine watumie kondom na pia alisema kuwa ni nzuri kwasababu itawapunguzia maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Kwa upande wa mganga mkuu wa halmashauri ya jiji Dr Ibrahim Isaack aliwapongeza kampuni hii ya PSI kwa kuwajali watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi na aliwashauri waendelee kusaidia watu kama hawa na kuwasihi na makampuni mengine yajitokeze kusaidia watu hawa ambao wanaishi na maambukizi kwani asilimia kubwa hawana uwezo.
Alisema kuwa kwa upande wa jiji la Arusha maambukizi ya virusi vya ukimwi yamefukia asilimia 4.3 kwa mwezi na hii inatokana na wingi wa watu wanaoingia na kutoka kila siku katika halmashauri hii ya jiji.
Alisema ili kupunguza ongezeko hili la maambukizi ya virusi vya ukimwi ni wajibu wa kila mtu kutambaa ugonjwa upo unauwa na kwa wale ambao wameathirika wajaribu kuwashauri waatu ambao hawaja adhirika na pia ni wajibu wa kila mtu kwenda kupima afya yake.
"unajua ni wajibu wa kila mtu akapime afya yake na iwapo atagundua mapema kuwa anamaambukizi haya afuate ushauri wa daktari na kama ataukubali mapema na kuufuata basi ataishi vyema na kwa muda mrefua zaidi ata ya yule ambaye ajapima"alisema Isaack.
Akipokea msaada huo katibu wa kikundi cha wanaoishi na matumaini cha Tupo Richardi Laizar alisema kuwa wameamua kuomba kondom hizi kwa kampuni hii ya PSI kutokana na kuona wakina mama wengi ambao wanaishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi ambao wapo katika vikundi vyao wamekuwa wakizaa bila mpango.
"unajua tuliona wanawake ambao wanaishi katika vikundi vyetu wanazaa kila siku ivyo tukaona njia pekee ya kupunguza ongezeko hili ni kutumia kondom ivyo tukaamua kuomba katika shirika hili na tunashukuru mungu wametambua umuhimu wetu wakatupa"alisema Laizar.
Naye meneja wa kanda wa PSi Robinson Katule alisema kuwa anapenda kuwashauri watu kutofanya ngono uzembe wakijua kukwa dawa ya ukimwi imepatikana bali wanatakiwa watumie kinga kila mara ili kuweza kujiepusha ugonjwa huu.
Alisema kuwa mpaka sasa hamna mtu ambaye ameshaiyona dawa hiyo na kama kweli ingekuwa imepatikana basi ingesha tangazwa rasmi na mamlaka husika na kusisitiza kuwa atakama dawa imepatikana maambukizi haya jaisha yatakuwepo ivyo kinachotakiwa ni kujilinda ili kutopata maambukizi haya.
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia