CHADEMA WACHARUKA JIMBO LA ARUSHA MJINI
Wito umetolewa kwa wakazi wa Jiji la Arusha kutambua kuwa sera madhubuti zinazoelekea katika uboreshaji wa
miundombinu ndio chachu kuu ya maendeleo ya taifa lolote lile.
Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mgombea wa ubunge Arusha Mjini kwa kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema Jonathani wakati wa mkutano wa adhara uliofanyika kata ya kijenge ,ambapo ulikuwa ni mkutano maluumu wa kunadi mgombea huyo wa ubunge pamoja na madiwani wanaowakililsha CHADEMA .
Lema alisema kuwa kwa sasa hivi Chama cha CHADEMA kipaombele kikubwa walichokipanafasi kubwa sana katika sera zao kwa jiji la Arusha na viunga vyake ni kuboresha Miundo Mbinu yote ndani ya jiji hili.
“Sisi CHADEMA tunaelewa kwamba tatizo lamiundo mbinu ndani ya jiji la Arusha ambapo haitoshelezi mahitajia ya wakazi wake ndio inayorudisha nyuma maendeleo ya wakazi wa jiji hili”, Alisisitiza Lema.
Alisema endapo wakazi wa jiji la Arusha watakipa ridhaa chama cha CHADEMA katika uchaguzi huu wataboresha mtandao wa Barabara sambamba na kuboresha madaraja ya kunganisha kata zote 19 za jiji la Arusha.
Aidha alisema Wanao mpango kabambe wa wakuboresha Hospitali mkoa Arusha Mount Meru iwe na hadhi kubwa kupita Hospitali za taasisi zilizopo nchini ikiwemo Seliani pamoja na Bugando.
Katika kuwezakutimiza hilo la ukarabati wa Hospitali hiyo ya Mount Meru wamepanga mapango wa kuwashawishi watumiaji wa simu mkoani Arusha wapatao Laki 4 kuchangia takribani shilingi 500 kawa mwezi ambapo wana uhakika wa kupata zaidi ya shilingi Milioni 100.
Pamoja na hayo alisema kuwa katika elimu Ndani ya jiji laArusha wana mpango wa kukuza kiwangocha elimu Sambamba na kuboresha masilahi Duni wanayopata walimu mkoani Arusha.
Lema alibainisha kuwa kwa mwaka huu chama chake kimejipanga vyema kulinda kura zao vilivyo ili wasije wakaibiwa kama uchaguzi uliopita walivyofanyiwa na alisisitiza kuwa kila mwananchi aende kupiga kura na achague kiongozi ambaye atafaa na atakae liletea jimbo lake na hata nchi kwa ujumla maendeleo.
"mwaka jana nilibahatika kushinda usiku na kura zikaonyesha nimeshinda sasa ilivyofika asubuhi eti nikanyanganywa madaraka na kuambiwa sikushinda afu hao hao wakaanza kunikashifu eti wamenipa ela nikawaachia madaraka ila kwa mwaka huu nimejipanga vyema kwani nimekomaa zaidi katika siasa na hawata niibia kura tena kama walivyofanya mwanzo"alisema lema
Alisema kuwa ni wajibu wakila kiongozi kuchagua matu anayefaa na atakaye weza kumuongoza vyema na kumletea maendeleo na kusisitiza kwa kuwaasa wananchi kutotoa kura zao kwa ajili ya kupiwa vitu vidogo kama kanga ,sukari na hata hela bali wapige kura kulingana na kumuangalia kiongozi anayemfaa na aangalie kama alikuwa kiongozi nini amewafanyia katika kipindi chake cha uongozi na wajiulize je wakimchagua atatimiza aliyoyahaidi au ndo baada ya kupata atatumia gari ya giza(tinteidi ) ili wananchi wasimuone na kumlilia shida .
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia