TIMU YA TAIFA YA RIADHA YAJIFUA


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Riadha Endro Boro akiwapa maelekezo wachezaji wake wakati wakifanya mazoezi ya kujiandaa kwenda nchi India katika mashindano ya kimataifa yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi October 3


Kocha mkuu wa Tanzania wa timu ya raadha Endro Boro amelalamikia uchache wa siku za mazoezi kwa timu ya taifa ambayo anaiandaa kwenda kwenye mashindano nchi india .

Akizungumza na lebeneke hili ndani ya kiwanja cha Sherk Amri Abeid kocha huyo amesema kuwa anasikitishwa sana na uchache wa siku ambazo amepangiwa kuiandaa timu hiyo ambayo inatarajiwa kuondoka jijini hapa Septembar 24 kwenda jijini Dar es salaam kwa ajili ya safari yao ya kwenda India.

Alisema kuwa amepewa wiki tatu tu kuiandaa hiyo timu ambayo inaenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa ya riadha kitu ambacho ni chache sana kulingana na wachezaji wenyewe.

"Unajua kuna mazoezi mengi sana vijana hawa walitakiwa wafanye kama kufanya mazoezi ya mikuki kuifanya mazoezi ya misuli,kwenda gym na hata kukimbia na kutengeneza speedi sasa mpka sasa wamefanya moja la kukimbi kimbia na bado hawajawa kama nilivyotaka yani nasikitika sana "alisema Boro

Alisema kuwa anaimani kabisa kama wangekuwa wamepata mda mrefu basi wangeweza kufanya vizuri zaidi na kufanya mazoezi yao vyema kwani wachezaji wake ni wazuri .

Alisema kuwa timu yake inajumla ya wachezaji tisa ambao wametoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ikiwemo manyara ,Kilimanjaro,Dodoma,Singida pamoja na mkoa wa Arusha.

Kwa upande wa raisi wa Chama cha riadha Tanzania France John alisema kuwa vijana hawa wamejiandaa vizuri licha ya kuwa kocha wao ameulalamikia mda wa mazoezi.

"Vijana wamejianda vyema sababu kabla ya kocha huyu anaewafundisha wa taifa kuanza kuwafundishi wachezaji hawa walikuwa wameshaanza kufanya mazoezi katika vilabu vyao hivyo nasema wako vyema kabisa kama ni mapungufu ni madogo tu nanathani katika siku hizi watakuwa wamerekebika na watafanya vyema"alisema john

Alibainisha kuwa mashindano ambayo timu hii inaenda kushishiriki ni magumu sana kwani wamekutana na watu mbalimbali wengi ila wamejiaanda vya kutosha.

Aliishukuru serekali kwa kuisaidia mchezo huu haswa katika safari hii kwani imeigaramikia wachezaji mambo mengi ikiwemo usafiri na hata malazi .



About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia