Wananchi wa Kijiji cha Elesin'geta kilichopo katika kata ya Mundarara wilayani Longido mkoani Arusha wametakiwa kuhakikisha wanatetea ,kuhifadhi na kutunza ardhi yao Kwa manufaa ya vizazi vijavyo kwani binadamu wanaongezeka lakini aridhi aiongezeki
Aidha pia vijana wa vijiji hivyo wametakiwa kufanya kazi Kwa bidii , kuhifadhi na kutumia fedha ambazo wanazipata Katika kazi zao vizuri katika kufanya shughuli za maendeleo na sio kufanya anasa ili kuweza kujikwamua katika wimbo la umaskini na kuliongezea pato taifa .
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa kampuni ya uchimbaji wa mdini ya rubby ijulikanayo kwa jina la SENDEU MINING LIMITED,Gabriel Sendeu Laizer wakati akiongea katika sherehe za kumsimika mwenyekiti wa kijiji hicho mstaafu kuwa chifu wa ukoo wa kipuyo (legwanani) Akwelino Nikeni pamoja na kumpongeza Kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati wa uongozi wake ikiwemo ya kuwasaidia wananchi wa Kijiji hicho kupata maeneo ya kuchimba madini hayo ya rubby.
Alisema kuwa ni vyema wananchi wa Longido wakaendelee kulinda na kuhifadhi vyema ardhi yao Kwa ajili ya kuvihifadhia vizazi vijavyo kwani iwapo wataitumia vibaya watasababisha watoto watakao zaliwa halo baadae kukosa aridhi ya kunitumia.
"Niwasihi pia vijana ambao mpo hapa mnaofanya shughuli zenu ikiwemo za uchimbaji madini mtumie fedha hizo vyema Kwa ajili ya maendeleo na sio mmalizie Kwa wanawake pamoja na kunywa pombe ,mkitumia vyema itawasaidia nyie wenyewe pamoja na vizazi vyenu pia itamsaidia kuongeza pato lataifa"alisema Sendeu
Aidha pia wachimbaji hao wa mkoa wa Arusha walimshukuru Rais Samia Suluhu Kwa kuwapatia wananchi wa wilaya hiyo maeneo Kwa ajili ya kuchimba madini hayo ambapo alisema kuwa maeneo hayo yameweza kuwapatia vijana wengi ajira na kuwaondoa kabisa katika umaskini
"Nimshukuru pia katibu Mkuu wa taifa wa ccm Daniel Chongolo pamoja na waziri wa madini Dotto Biteko kwakuwa wao wamesaidia sana sisi wananchi wa longido kupewa maeneo haya Kwa ajili ya kufanya kazi hii ya uchimbaji ambayo kwakweli imesaidia sana vijana wengi kupata ajira"alisema Sendeu
Aidha pia Sendeu katika kutambua mchango wa Mwenyekiti mstaafu wa Kijiji hicho wa kufanya kazi nzuri katika kipindi cha uongozi wake aliweza kumkabishi nyumba aliyomjengea pamoja na gari aina ya Noha aliyomnunulia Kwa ajili ya shukrani.
Akitoa shukrani zake mwenyekiti hiyo mstaafu wa Kijiji hicho Akwelino Nikeni aliwashukuru sana wananchi Kwa namna walivyotambua mchango wake alioutoa wa kusaidia jamii katika kipindi cha uongozi wake ambapo aliwahaidi kuendelea kuwapa ushirikiano hata katika kipindi ambacho ayupo katika uongozi.
"Nimshukuru pia Sendeu Kwa kunipa gari hii niahidi tu gari hii mbali na matumizi yangu binafsi pia litatumika kuwasaidia wananchi wa Kijiji hiki na kata hii pindi watakapo kuwa na uhitaji wowote pia nyumba hii itanisaidia kuishi Mimi na familia yangu
"alisema Nikeni
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli Isack Copriano aliwataka wananchi wa wilaya ya longido kushirikiana kutunza udongo wa Tanzania maana hakuna hazina nyingine yoyote iliopo au watakao weza kupata zaidi ya ardhi.