Mtalamu wa kutengeneza mashine kutoka Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) Mosses Chalamila akiwaelezea Wakulima waliouthuria katika maonyesho ya nane nane Kwa upande wa Kanda ya kaskazini yanayofanyika katika viwanja vya Themi njiro mkoani Arusha namna mashine ya kukamua mafuta ya maweze iliobuniwa na taasisi hiyo inavyofanya kazi (Woinde Shizza).
Woinde Shizza, ARUSHA
KATIKA kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa vifaa tiba nchini, Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) imeanzisha karakana yakisasa kuzalisha vifaa tiba kwa ajili ya hospitali pamoja vituo vya afya hapa nchini.
Hayo yamekuja baada ya kipindi cha mwaka 2021/2022 ambapo taasisi hiyo iliamua kuwekeza zaidi ya Shilingi bilioni tatu kwa ajili karakana ya kisasa yakutengeneza vifaa tiba aina 17 Mpaka sasa baadhi ya vifaa tiba vimeshazalishwa
Hayo yamebainishwa na Afisa mawasiliano na masoko Dkt. Sigisbert Mmasi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika Maonesho ya Wakulima Nanenane yanayofanyika katika Viwanja vya Themi- Njiro, jijini Arusha ambapo alisema kuwa taasisi hiyo inamalengo makuu matatu ikiwemo kufanya tafiti zitakazotoa suluhu ya matatizo yaliopo katika jamii.
Aidha pia alisema wanatoa mafunzo ya kihandisi kwa watu ambao wanafanya kazi ndani ya viwanda kwaajili ya uendeshaji, usalama viwandani pamoja mambo mbalimbali yanayohusiana na uzalishaji tija Viwanda.
Alisema kuwa TEMDO inatengeneza vifaa tiba kwa ajili hospitali, zahanati, vituo vya afya nchini lengo likiwa ni kupunguza uingizwaji wa vifaa kutoka nje ya nchi pamojana kupunguza matumizi ya fedha za kigeni.
“katika maonyesho haya tumekuja kuonyesha vifaa tiba ambayo vinatengenezwa TEMDO pamoja na kutoa elimu kwa Wakulima na wananchi waliohudhuria maonyesho haya ya nane nane tunaamini kwamba watakuwa mabalozi wetu waziri wa kututangaza temdo na kuja kununua bidhaa zetu,"alisema
Alibainisha kuwa tayari taasisi hiyo imeweka mikakati mbalimbali kuhakikisha kuwa inazalisha vifaa vya kutosha
Alitaja baadhi ya vifaa hivyo wanavyovitenga kuwa ni pamoja na vitanda vya wodi ya wajawazito, stendi za kuwekea drip,vitanda vya wagonjwa kufanyiwa uchunguzi pamoja na vitanda vya wagonjwa wanaolazwa ,jokofu la kuhifadhia maiti pamoja na kiteketeza uchafu wa hospitalia,ambapo alibainisha kuwa
karakana hiyo kwa sasa inauwezo wakutengeneza vitanda zaidi ya 500 vya wajawazito na vitanda na vya wagonjwa wanaolazwa hospitalini.
“Taasisi yetu pia tunazalisha majokofu yakuhifadhia maiti, pia tunatengeneza viteketezataka za mahospitali, hivyo tunakaribisha wadau wa afya na wamiliki wa hospitali binafsi za Serikali , zahanati na vituo vya afya kununua vifaa tiba katika taasisı yetu"alisema Dr Mmasi
"Watanzania wenzangu ikiwemo wizara ya afya ,zahanati , hospital za serikali pamoja na binafsi niwatake tu kutumia vifaa tiba vinavyoendana na uhalisia wa kitanzania vinavyotengenezwa na taasisi ya ubunifu na usanifu mitambo (TEMDO)Kwani vinadumu muda mrefu na kwakutumia vifaa vinavyotengenezwa ndani ya nchi vinasaidia kutokutumia fedha za kigeni Kwaajili ya kuagiza nje ya nchi ambayo ni gharama kubwa"alisema Dr Mmasi.
Aidha alisema kuwa mbali na vifaa tiba pia TEMDO wametengeneza mashine za aina mbalimbali za kilimo, viwandani pamoja na kutoa elimu kwa wahandisi na mafundi uch
undo nchini