Mwalimu Sifael Shuma, Je mnamkumbuka ? Kuwakumbusha tu ni mmoja ya wanawake wawili walioshika vibuyu vyenye udongo uliochanganywa wakati wa siku ya Muungano wa Tanzania tarehe 26/04/1964.
WASIFU WAKE
-Mwalimu wa kwanza Mtanzania katika Machame Girls Secondary School mwaka 1959
-Mkuu wa shule kuanzia mwaka 1970 mpaka alipostaafu mwaka 1993.
-Baadaye aliombwa kwa mkataba kuwa mkuu wa chuo cha Hai Vocation training centre kuwa mkuu mpaka 2008.
-Kwa hivi sasa anasaidia utawala na uendeshaji wa hoteli ya moja ya kitalii iliyopo machame
Tags
habari matukio