BREAKING NEWS

Monday, May 30, 2011

JKT OLJORO YASAJILI WATANO

Timu ya Jkt Oljoro ya mkoani hapa ambayo inatarajia kushiriki ligi kuu msimu ujao imesajili wachezaji watano kwa ajili ya kuongezea nguvu timu hiyo ambao wametoka katkika vilabu mbalimbali hapa nchini.

Wachezaji hao ambao wamesajili kutoka katika klabu za Rhino ya Tabora ,Villa squaa,pamoja na Tmk wameingia kambini na wapo na wenzao katika mazoezi makali kwa ajili ya kujifua ili kuweza kushiriki ligi kuu msimu ujao ambayo inatarajiwa kuanza kutimu vumbi mapema mwenzi wa nane mwaka huu.

katibu wa timu hiyo Alex Mamgaya alisema kuwa wachezaji ambao wamesajiliwa ni pamojas na Mohamed Nonga kutoka timu ya Rhino ya Tabora,Mecky Maiko kutoka timu ya Villa squid.

Wengine waliosajiliwa ni Paulo Malipesa kutoka timu ya TMK na mwenzake Rashid Nasoro naye akiwa ametoka katika timu hii hii ya TMK.

Alisema kuwa wao kama klabu wanatarajia kusajili waachezaji tisa laikini hii ndio hawamu ya kwanza ambayo wamesajili ambao wamesajili wachezajui watano na wamebakiza wachezaji wanne ambao wao wapo katika mazungumzo kwaaajili yakuwasajili.

Aidha alisema kuwa wao hawajaacha mchezaji hata mmoja ambaye alisaidia kupandisha timu katika msimu uliopita ila kunamchezaji mmoja ambaye yeye alichukuliwa na timu ya Simba ambaye amemtaja kwa jina la Nasor Choro .

Alisema kuwa kwa upande wa timu yake wote wako vizuri na wacheza wako kambini wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na ligi kuu huku akisisitiza kuwa wanaimani kwa mwaka huu wataweka historia kwa mkoa kwani hawatashuka daraja tena.

"unajua mazoezi tunayoyafanya nauhakika kabisa tutabaki katika historia kwani wachezaji wetu ni wazuri ,walimu ni wazuri hivyo lazima tubakie ligi kuu bwana watu walizoea timu za Arusha zinapanda na kushuka lakini msimu huu wasahau lazima tubaki ili tuweke historia"alisema Mamgaya.

Alisema kuwa malengo yao ni kuchukuwa ubigwa na bila kupewa ushirikiano na wadau wa arusha itakuwa ngumu hivbyo aliwaomba wadau wa soka wa mkoa huu kujitokeza kwa wingi kuisaidia timu hiyo kwani pamoja na mazoezi wanayo yafanya pia wanaitaji nguvu kutoka kwa wadau.

Timu hii ya JKT Oljoro ipo kambini na imeweka kambi yake katika viwanja vya nane nane vilivyopo njiro mkoani hapa.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates