BREAKING NEWS

Monday, May 30, 2011

MABENKI YATAKIWA KULEGEZA MASHARITI YA MIKOPO


Wito umetolewa kwa makampuni pamoja na benki zinazotoa mikopo kulegeza mashariti ili kuweza kuwa saidia wafanya biashara kuweza kuefanya biashara zao kwa umakini.

hayo yalibainishwa na mkurugenzi wa kampuni ya maua ya Mounti Meru Flower Herwig Tretter wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake.

Alisema kuwa makampuni mengi pamoja na viwanda vimekuwa vinashindwa kuendelea kutokana na mashariti magumu ambayo wanapewa wakati wanapokwenda kuchukukwa mikopo.

"unajua makampuni mengi yamekuwa yanategemea mikopo sasa mtu ukichukuwa mkopo unakuta unapewa mashariti magumu sana hali ambayo inasababisha hata kushindwa kuendeleza biashara"alisema Tretter.

Alibinisha kuwa wamekuwa wakichukuwa mikopo kwa ajili ya kuendeshea biashara zao lakini mwisho wa siku wanakuta hawapati faida yoyote kwani faida wanayopata badala ya kuzungusha biashara wamekuwa waki rudisha mikopo hiyo.

Alisema kuwa kuna makampuni mengi pamoja na viwanda ambavyo vilikuwa vikiendeshwa na mikopo hiyo na kwasasa vimefungwa kutokana na kushindwa kulipa marejesho ya mikopo waliyochukuwa.

"kunaviwanda vingi vimefungwa kama vya maua vipo vinafungwa kulingana na wamiliki kushidwa kulipa kulipa mikopo ambayo walichukuwa hivyo tukiendelea hivi itafikia hatua tutaishiwa makampuni pamoja na viwanda "alisema Tretter

Tretter alisema kuwa anawaomba sana mabenki yanayotoa mikopo kulegeza mashariti yao ili kuweza kuwafanya wafanyabiashara mbalimbali kuweza kujiendeleza kupitia mikopo hiyo.

Alisema kuwa iwapo watarahisisha mikopo itawaafanya wao kuweza kufanya biashara kwa kiwango cha hali ya juu zaidi tofauti na sasa wanakuwa wanapata kazi nyingi lakini wanashindwa kuzifanya kutokana na kukosa fedha za kufanyia kazi hizo.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates