BREAKING NEWS

Monday, May 23, 2011

MALIPO YA MKANDARASI WA BARABARA YA NAMANGA -ARUSHA YASITISHWA


Injinia kutoka nchini china ambaye ndo anatengeneza barabara ya Namanga -Arusha Wang Ruiri akiwa anampa maelekezo Naibu Katibu mkuu wa wizara ya miundo mbinu Eng.Dr. John Ndunguru wakati alipokuwa anakagua barabara iyo.



Meneja Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Arusha Deusdedit Kakoko akiwa anaongea na wakandarasi wa barabara ya Arusha namanga


Naibu Katibu mkuu wa wizara ya miundo mbinu Eng.Dr. John Ndunguru aliyevaa suti nyeusi akiwa anampa maelekezo mkandarasi wa barabara ya Namanga-Arusha Wang Ruiri wakati alipotembelea barabara hiyo


Wizara ya ujenzi imesimamisha malipo ya kilometa 16 kwa mkandarasi anayejenga barabara ya Arusha –Namanga kutokana na kugundulika kwa makosa katika maeneo ya maungo ya barabara hiyo .



Aidha wizara hiyo imemtaka mkandarasi wa barabara ambaye ni China Geo-Engineering Corporation kuharakisha ujenzi huo haraka ili barabara hiyo iweze kukamilika katika muda uliopangwa.



Barabara hiyo ambayo ina jumla ya kilometa 104 ambayo ilitakiwa kukabidhiwa mapema mwanzoni mwa Mwezi July mpaka sasa bado haijakamilika na jumla ya kilo meta tano bado hazijawekewa lami na matengenezo hayaja isha mpaka kufikia sasa.



Akiongea kuhusiana na barabara hiyo Naibu Katibu mkuu wa wizara ya miundo mbinu Eng.Dr. John Ndunguru wakati aliopotembelea barabara hiyo alimtaka mkandarasi huyo aongeze kasi kubwa ili kuweza kukabidhi barabara hiyo katika kipindi kilichopangwa .



“napenda kukwambia kuwa ukazani ujitaidi uwezavyo na sio kujitaidi kwako ufanye mradi tunataka barabara ikabidhiwe mapema iwezekanavyo katika muda uliopangwa ili viongozi nao waweze kuona barabara yao ikiwa imekamilika na inaubora wa kutosha”alisema Ndunguru.



Aidha aliwataka warekebishe maungo ambayo yameonekana yanamatatizo katika baadhi ya sehemu ya barabara hiyo ili kuweza kufanya barabara iwe na kiwango cha hali ya juu na kuweza kudumu kwa muda mrefu.



“tunataka barabara iwe nzuri sio mfanye rafu mkija kutukabidhi tunakaa siku mbili tatu unakuta barabara imeharibika kwaiyo jitaidini malizieni sehemu zilizobaki na pia akatika sehemu ambazo kunamakosa mrekebishe tukipita tena uku tuweze kuridhishwa na barabara na iwe na kiwango”alisema Ndunguru.



Kwa upande wake mkandarasi wa barabara hiyo Wang Ruiri alisema kuwa waomesikia na watafanyia marekebisho sehemu ambazo zinamatatizo .



Pia alisema kuwa watajitaidi kadri watakavyo weza waikabidhi barabara hiyo katika kipindi kilichopagwa japo kuwa wawezi kusema watakabidhi siku iyo iyo au la.



Naye Meneja Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Arusha Deusdedit Kakoko alisema kuwa ataendelea kufuatiali barabara hiyo na hata hakikisha inaisha katika mda unaotakiwa.



Alisema kuwa ujenzi unaendelea vizuri katika barabara hiyo na ila kwa upande wa hizo kilometa 16 ambazo zinamakosa atazisimamia na kuhakikisha zinafanyiwa marekebisho ya kutosha.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates