Ticker

6/recent/ticker-posts

KILI TAIFA CUP YACHACHAMAA MKOANI KILIMANJARO


Apa baadhi ya waandishi waliokuwepo kwenye mashindano hayo na dada Woinde alikuwepo wa katika kati



Wachezaji wa timu ya Arusha wakirudi na kupokelewa na mashabiki huku wakipongezwa mara baada yakumaliza mechi ambayo waliwafunga timu ya Tanga magoli 3-1


Goli kipa wa timu ya Mkoa ya Arusha Mohamed Hamis akiwa anaongea na golikipa mwenzake ambaye alikuwa golini siku iyo Aldina Hashim aliyevaa orange wakati wa mapumziko



Mchezaji wa timu ya mkoa wa Tanga aliyevaa nyekundu akikabana na mchezaji wa timu ya Arusha alivaa kijani


Kocha wa timu ya Mounti Meru Woirrius akiwa anawapa maelekezo wachezaji wake

Timu zote zikiwa tayari kuingia uwanjani



Timu ya mkoa wa Kilimanjaro

Timu ya soka mkoa wa Arusha Mounti Meru Worriasi imeweza kutoka kifua mbele mara baada ya kuichapa timu ya soka ya mkoa wa tanga Tanga stax mabao 3-1.

Mchezaji Abudalah Juma wa Mounti meru aliweza kuipatia timu yake goli la kwanza la kufungua dimba kunako dakika ya pili baada ya mchezaji Hamis Mroki aliweza kuipatia timu yake goli la pili kunako dakika ya nne magoli ambayo yalitawala hadi kipindi cha kwanza kumalizika .

Kipindi cha pili kilianza vyema na timu ya mkoa wa Tanga ilionekana kurudi na nguvu za kutaka kusawazisha magoli hayo na ilipotimu kunako dakika ya 84 Salim Azizi Gila aliweza kuipatia timu ya tanga goli la kufutia machozi mara baada ya kuwaponyoka walinda mlango wa timu ya Arusha na kupiga shuti kali.

Mchezo uliendelea na mchezaji wa timu ya Arusha Abudala Juma aliweza kuiongezea timu yake bao la tatu kunako dakika ya 89 dakika moja kabla ya kipenga cha mwisho kupulizwa na mwamuzi kutoka dar Omari Yusuph Arusha kuibuka kidedea cha magoli 3 huku tanga ikiongoka na goli moja 3-1.

katika mechi ingine ambayo ilichezwa katika uwanja huo wa Jamuhuri timu mwenyeji wa mashindano haya ya Kili taifa cup kilimanjaro stax iliweza kuanza vibaya mashindano haya mara baada ya kufunga bao 1-0 na timu Taifa ya vijana chini ya miaka 23.

Vijana hao chini ya miaka 23 wakiwa chini ya ungalizi wa kocha wao Jamhuri kiweni (julio) iliweza kupata goli la kwanza katika dakika ya 52 katika kipindi cha pili mara baada ya mchezaji wao thomas ulimwengu kuwasambaratisha mabeki wa timu ya kilimanjaro na kupiga shuti kali iliyonda mlinda mlango wa timu ya kilimanjaro na kumuacha akiwa ameduwaaa.

japo kuwa timu hii mwenyeji ya kilimanjaro ilifikia hatua ya kucheza pungufu ya mchezaji mmoja mara baada ya mchezaji wake dole mgono kupewa kadi nyekundu mara baada ya kumchezea rafu mchezaji wa timu ya vijana ya taifa chini ya miaka 23 lakini pia timu hii ya kilimanjaro iliweza kupata nafasi nyingi za wazi lakini ilishindwa kuzitumia hali iliwasababishia hadi kipenga cha mwisho kupulizwa na mwamuzi wa mchezo huu Andwer shamba timu ya vijana iliibuka kidedea cha goli 1-0.

Nilizungumza na kocha wa timu ya Arusha Madaraka bendera alisema kuwa yeye binafsi anaamini kikombe kitaenda arusha kwani vijana ambao amewaandaa ni wazoefu wa michezo na amewapa mazoezi mazuri japo kuwa waliwaweka kambini kwa muda wa wiki mbili tu.

Kwa upande wake katibu msaidizi wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Arusha Geradi munis alisema kuwa mashano ni mazuri ila kitu kinachowaangusha ni uwanja kwani uwanja ni mbovu sana hali ambayo inasababisha timu yao kupoteza magoli mengi sana.

Alitoa wito tena kwa wathamini wa kuu wa mashindano haya kuwaongezea fedha za uzamini kwani fedha ambazo wanawapa ni ndogo sana kiasi kwa hata wachezaji wenyewe wanakosa posho.

"unajua kilimanjaro wanatuzamini sawa tunashukuru lakini fedha ambazo wanatupa ni ndogo hazitoshi yaani fedha hizi hata wachezaji wenyewe hawapati posho afu kibaya zaidi tunashindwa kupata watu wa kutusaidia timu kwakuwa ukienda unaambiwa kwani kilimanjaro si wamethamini wamewapa ela nyingi ivyo tunaomba watuangalie sana katika msimu ujao''alisema Geradi.






Kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Meja Jenerali Said Kalembo
akisalimiana na wachezaji wa timu ya taifa ya vijana U-23.

Kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Meja Jenerali Said Kalembo
akisalimiana na wachezaji wa timu ya taifa ya vijana U-23.


Timu ya vijana kabla ya kuingia uwanjani kukipiga na timu ya mkoa wa
kilimanjaro na

Post a Comment

0 Comments