BREAKING NEWS

Monday, May 30, 2011

RHINO YAUZWA

Timu ya Rhino ya mkoani hapa imetangazwa rasmi kuuzwa na mmiliki wake kutokana na kukosa viongozi wa kuingoza atimu hiyo .

Akiiongea na waandishi wa habari mkoani hapa mmiliki wa timu hiyo ambaye pia ni mmiliki wa timu ya Bishop durning ambayo inashiriki ligi ya wilaya Sarubare Lendisa alisema kuwa yeye ameamua kutangaza rasmi kuuza kwa timu hiyo kutokana na kukiosa viongozi wazuri wakuingoza timu hiyo.

Alisema kuwa awali alinunua timu hiyo akiwa na nia ya kuwazawadia wakazi wa mkoa wa Arusha ili waweze kushirikiana na kuwa natimu nyingi zinazoshiriki ligi kuu lakini amesikitishwa na kitendo cha uongozi wa soka wa mkoa wa Arusha pamoja na wadau kutompa ushirikiano.

"Nilinunua timu hii kwa nia ya kuwazawadia wakazi wa mkoa huu pia nilikuwa na jua watanipa ushirikiano ili ata mkoa wetu uwe na timu nyingi lakini imekuwa sivyo kwani hawajanionyesha ushirikiano wowote"alisema Lendisa.

Alisema kuwa walipata viongozi ambao walion goza timu hii katika kipindi cha mwanzo wakawaamini lakini walipo wakabidhi timu walibadilika na kutofanya mambo ambayo alitarajia kwani walianza kuuuza mechi nyingi hali ambayo ilipelekea ata timu hiyo kuishia katika mzunguko wa kwanza.

"hawa viongozi waliokuwa awali nimewapa timu nikajua watafanya vyema lakini matokeo yake wameenda uko wakawa wanakaa na kunywa wakasababisha ata timu haijaingia katika hatua ya tisa bora"alisema Lendisa.

Aidha aliwataka wadau mbalimbali wa michezo wakiwemo taasisi za serekali na binafsi ,makampuni,watu binafsi na hata vilabu mbalimbali ambao watataka kununua timu hiyo kujitokeza katika uongozi ili waweze kuichukua timu hiyo.

Alibinisha kuwa timu hiyo haina matatizo yoyote kwani inamilikiwa na mtu mmoja na pia haina madeni yoyote kwani walisha yalipa yote.

Timu hii ya Rhino awali ilikuwa inamilikiwa na chama cha mpira wa miguu mkoani Morogoro lakini iliuzwa na chama hicho na kwa sasa inamilikiwa na Sarubare Lendisa wa mkoani |hapa.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates