Ticker

6/recent/ticker-posts

MSHINDI WA KCB GOLF EAST AFRIKA 2011 KUONDOKA NA ZAIDI YA MILIONI TATU



Ratiba ya KCB golf East Africa Tour 2011


Mchezaji wa golf akiendelea na mashindano






Mkuu wa idara ya masoko na mahusiano wa benki ya Kcb Christina Manyenye akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Arusha Gymkana klabu wakati wa uzinduzi wa mashindano ya KCB eastafrikan Golf Tour 2011 kulia kwake ni mwenyekiti wa Gofu Arusha Gymkana Klabu Richard Gomes kushoto kwake ni mwenyekiti wa maprofeshinal gofu kutoka nchini Kenya Charan Thethy


Profeshinal gofu wa mashindano ya Kcb East Africa Golf Tour 2011yanayofanyika jijini hapa katika viwanja vya Arusha Gymkana Klabu anatarajia kuondoka na kitita cha shilingi lakimbili za Kenya ambayo ni sawa na shilingi milioni 3,630,000 za Kitanzania.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa idara ya masoko na mahusiano wa benki ya Kcb Christina Manyenye wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na mshandano haya yanayotarajia kuanza leo (jumatano ) na kufikia tamati yake jumamosi.

Alisema kuwa wao kama Kcb benki wameamua kuaandaa mashindano haya ya gofu lengo kuu likiwa ni kukuza vipaji vya wachezaji ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kutangaza benki hiyo kwa nchi za jumuiya.


Alisema kuwa wao kama KCB hii ni mara yao ya pili kuthamini mashindano haya kwani mwaka jana pia walithamini mashindano kama haya ambapo alisema kuwa mashindano haya yanafanyika katika nchi za Est Afrika na katika kila nchi kunateuliwa klabu moja ambayo itaweza kuyaendesha mashindano haya ikiwa ni pamoja na kuandaa.

Alisema kuwa mpaka sasa jumla klabu tatu zimeshafanya mashindano haya ambapo kwa nchi ya Tanzania ni yanne ambapo wameteuwa Arusha Gymkana Klabu kama wenyeji wa mashindano haya.

''mpaka sasa tumefanya katika klabu tatu ambazo ni Thika golft klabu ,Muthanga golf klabu ,Nyanza golf klabu na sasa ni Arusha Gymkana Klabu na tukituoka hapa tunatarajia kufanya katika klabu ya Kigali golf Klabu,Nakuru golf klabu ,Uganda golf klabu pamoja na Nyali golf ambapo katika klabu hii ya Nyali ndipo tutakapo fanya fainali zote hapo"alisema Manyenye.

Alibainisha kuwa mara baada ya mashindano haya nchi zote yaani Klabu zitaenda kushiriki mashindano ya fainali ambao yatafanyika katika klabu ya Nyali nchini Kenya.

Alisema kuwa wao kama Kcb benki wanatarajia kutumia zaidi ya shilingi milioni 78 za Kenya hadi kumalizika kwa mashindano haya.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Arusha Gymkana Klabu Richard Gomes aliishikuru benki hiyo ya Kcb kwa jinsi wanavyo jitolea kudhamini mashindano na mchezo wa golf kwa ujumla na aliwasihi waendeleee kuthamini na michezo mingine.

Alisema kuwa mpaka sasa jumla ya wachezaji 45 wanashiriki mashindano haya ambayo yamedhaminiwa na Kcb benki na alisema kuwa katika wachezaji hao wachezaji 30 wametoka nchini Kenya,10 ni wenyeji ambao ni Tanzania ,watatu kutoka Rwanda ,mmoja Ethiopia na mungine mmoja kutoka Uganda.

Gomes alisema kuwa nchi ya Burundi haijashiriki mashindano haya kwa sababu nchi hiyo bado inajitegemea katika mchezo huu lakini wapo katika mchakato wa kuingia katika mashindano yajayo mwakani.

Alitoa wito kwa wananchi mbalimbali kujitokeza kushiriki mchezo huu kwani mchezo huu sio wa matajiri kama wanavyofikiria bali ni wawatu wote.




Picha ni Mwenyekiti wa golfu wa Arusha Gymkana klabu Richard Gomes akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Kcb estafrika tour 2011

Post a Comment

0 Comments