Ticker

6/recent/ticker-posts

MURO AWAAIDI WATUMISHI WA MERU KUWAPA USHIRIKIANO


 mkuu wa wilaya ya Meru  mheshimiwa Jerry Muro akiongea na
watumishi wa halmashauri ya Meru
 aliekuwa kaimu  mkuu wa wilaya ya Meru ambaye sasa
ni Mkuu wa Wilaya ya Monduli mheshimiwa Idd Kimanta akizungumza wakati
wa kikao cha kumtambulisha mkuu wa wilaya ya meru kwa watumishi wa
halmashauri .
 Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakiwa kwenye kikao
Na Woinde Shizza,Arusha

Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru, mheshimiwa Jerry Muro  amwaadi
watumishi wa halmashauri ya meru kuwapa  ushirikiano wa  kuweza
kutimiza majukumu yao  ikiwa ni njia moja wapo huduma bora kwa
wananchi .



Hayo aliyasema wakati  alipokuwa akizungumza na wafanyakazi ,
watumishi  wa halmashauri  hiyo mkutano uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa halmashauri hiyo ambapo aliwahaidi kuwapa ushirikiano
watumishi wote katika swala zima la kusikiliza na kutatua  kero za
wananchi



" napenda kuwatoa hofu watumishi wote  kwa ujio wangu  kwani nitawapa
ushirikiano na kuwawezesha kutimiza majukumu yenu  ikiwa nipamoja na
utoaji wa huduma bora ili kutimiza azma ya Serikali ya awamu ya tano
ya kusikiliza na kuzitatua kero za wananchi pamoja na rasilimali za
Tanzania ili  kuwanufaisha wananchi wote hasa wanyonge na watoto wa
maskini, nukuu nimekuja hapa kutimiza torati na si kuivunja" Alisema
Muro.



Aidha alisema kuwa  ushirikiano huo utaanza kwa kuwapa fursa watumishi
hao kwa  kueleza changamoto zao na kupokea mawazo,maoni na mikakati
itakayoleta maendeleo kwenye Halmashauri hiyo na Wilaya ya Arumeru
ambapo alibainisha kuwa anatarajia kufanya kikao kingine mapema
jumatatu august 6 2018.



Awali aliyekuwa  akikaimu nafasi hiyo ambaye kwa sasa ni mkuu wa
wilaya ya Monduli Idd Kimanta akimkabidhi ofisi hiyo alisema kuwa
watumishi wa meru ni wazuri na wachapakazi na amemkabidhi pamoja na
ofisi wakiwa weupe na wenye Afya tele wanyeye kevu  wachapakazi .



Aidha aliwawataka watumishi hao kumpa ushirikiano mkubwa mkuu huo mpya
wa wilaya  kama walivyo mpa yeye  ili kuweza kuwaletea maendeleo
wananchi  wa meru na  taifa kwa ujumla.






Post a Comment

0 Comments