Ticker

6/recent/ticker-posts

Waziri wa Kilimo ataka kampuni za uwindaji wa Kitalii kuongeza michango kwa jamii





  waziri wa kilimo dk Charles Tizeba akizungumza na wafanyakazi  wa taasisi ya friedkin conservation fund ambayo  inamiliki  vitalu kadhaa vya uwindaji
Waziri wa Kilimo,Dk Charles Tzeba amezita kampuni za uwindaji wa kitalii nchini,kuongeza michango ya fedha wanazotoa kwa jamii ambayo inazunguka mapori ya akiba nchini.

Akizungumza na watendaji wa Taasisi ya uhifadhi ya Friedkin conservation Fund,(FCF) inayomiliki kampuni za uwindaji wa kitalii,katika maonesho ya Nanenane kitaifa mkoa Simiyu,Dk Tzeba alisema kuna kampuni zinapata fedha nyingi lakini uchangiaji jamii ni ndogo.

"Nyie najua mnafanya vizuri lakini wenzenu katika maeneo mengine hadi wamefikia hatua ya kuwachagulia miradi wananchi" alisema.

Hata hivyo,Afisa uhusiano wa FCF,Clarence Msafiri alisema kampuni zilizo chini ya Taasisi hiyo,zimekuwa zikitoa kwa jamii asilimia 20 ya mapato yao kila mwaka.

Alisema kampuni zao ikiwepo Mwiba Holding na TGTS na walizowekeza wilayani Meatu pori la Akiba la Maswa na Makao licha ya kutoa michango ya kijamii pia kwa mwaka wanatoa kwa vjiji zaidi ya sh 610 million kama kodi ya pango.

Naye Meneja ujirani Mwema wa kampuni ya Mwiba Holdings Alfred Mwakivike alisema kampuni hiyo kabla ya kusaidia miradi imekuwa ikipata maelekezo ya halmashauri.

"Miradi ambayo tunaitekeleza ambayo ina thamani zaidi ya sh 2. bilioni yote imeidhinishwa na halmashauri ya Meatu" alisema.

Taasisi ya Friedkin inashiriki maonesho ya nanenane kwa mara ya kwanza ili kuhamasisha uhifadhi,kupiga vita ujangili lakini kuonesha umuhimu wa mahusiano ya uhifadhi na kilimo.

(picha )

Post a Comment

0 Comments