Waziri wa fedha na mipango Dr.Philip Mipango akisalimiana na mwenyekiti wa bodi ya manunuzi Dr. Hellen Bandiho wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wabobezi na wanunuzi wa umma hii leo uliofanyika katika ukumbi wa simba uliopondani ya jengo la mikutano la AICC .
dr.philip mpango akifungua mkutano wa bodi ya manunuzi hii leo jijini arusha mkutano ambao unafanyika kwa siku tatu
Washiriki wa mkutano huo wakiwa wanafatilia mkutano huo kwa makini wakati waziri akifungua
waziri mpango akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa taasisi zilizopo chini ya taasisi ya wizara ya fedha na mipango
|
Na Woinde Shizza ,Arusha
Wataalamu wa manunuzi ya Umma nchini wametakiwa kuzingatia weredi katika utendaji wao wa kazi na kuepukana na vitendo vya ubadhilifu ,rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma jambo litakalosaidia kudhibiti matumizi mabaya ya fedha na kusaidia fedha hizo kutumika katika maendeleo mapana zaidi ya Taifa.
Akiongea kwa niaba ya Rais John Magufuli,wakati alipokuwa akifungua mkutano wa siku tatu wa wataalamu na wabobezi wa manunuzi ya umma(IPPC) kutoka nchini 46 duniani unaofanyika jijini Arusha,nchini Tanzania,waziri wa fedha na mipango dkt.Philp Mpango amesema mkutano huo unalenga kujadiliana namna ya kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma kupitia taknolojia mpya ya manunuzi .
‘’Ununuzi wa umma ndio sehemu kubwa ambapo fedha za bajeti zinapita hivyo ukifanyika vibaya maana yake serikali inapata hasara ndio maana tunasisitiza weredi wa wataalamu wa manunuzi kwa sababu kuna mamunuzi hewa na miradi hewa ’amesema dkt Mpango
Aidha amesema asilimia 70 ya fedha za matumizi ya kawaida zinapitia ununuzi wa umma na asilimia 100 ya bajeti ya fedha zote za maendeleo zinapitia manunuzi ya umma ,hivyo bajeti zote katika maeneo hayo mawili zikitumika vibaya lazima serikali iumie.
Amesema wataalamu wa manunuzi ya Umma wakitumia vizuri taaluma yao itasaidia maeneo mengine ya sera katika kukuza viwanda na kuinua sekta binafsi hivyo ununuzi utumike vizuri ili kusaidia kuinua nchi za afrika ikiwemo Tanzania kuendana na teknolojia iliyopo.
Awali Mwenyekiti wa bodi ya manunuzi ya umma nchini,dkt Hellen Bandiho amesema taasisi yao imeanza kuchukua hatua kwa wataalamu wake wasiozingatia weredi na maadili katika kazi zao na kuwataka waajiri kuhakikisha wanachukua wataalamu wa manunuzi ya umma wenye usajiri wa bodi yao.
‘’Wataalamu wa manunuzi ya umma wasio na usajiri ambalo wameajiriwa ama kufanya kazi zao bila usajiri ni makosa kwao na kwa mwajiri aliyewaajiri na hatua kali zitachukuliwa’’Amesema dkt Bandiho
Alivitaka vyombo vya dola kama polisi,takukuru na mahakama kushirikiana katika kuwaibuka na kuwachukulia hatua watu hao ambao wamekuwa wakiipaka matope bodi hiyo kwa kuendesha shughuli zako kinyume cha sheria.