Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII YARIDHISHWA NA UJENZI WA MAABARA TENGAMANO TAEC ARUSHA

Na Woinde Shizza, ARUSHA

 Kamati ya kudumu ya Bunge huduma na Maaendeleo ya jamii imetembelea Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kukagua mradi wa ujenzi wamaabara changamano awamu ya pili ambapo umekamilika kwa asililia 97%



Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji
 wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Prof. Lazaro Busagala aliiambia Kamati hiyo kuwa TAEC iliingia mkataba wa miaka 3 na kampuni ya Li Jun Development Constraction Company Ltd.16septemba 2019ambapo ujenzi huo uanatarajia kugharimu jumla ya kiasi cha Tsh. Bil.10.4 ambapo unatarajiwa kukamilika ifikapo 22septemba 2022

Prof Busagala amesema Ujenzi huo wa maabara utakapokamilika utawaongezea tija katika sera ya Taifa ya teknolojia ya nyuklia ya mwaka 2013 pia kusaidia sekta ya viwanda toambayo katika maeneo mbalimbali inategemea sana teknilojia hiyo ambayo ipo duniani, na usalama wa mionzi pamoja na wale wanaotengeneza vifaa vya mionzi

"Kwa sasa kuna zaidi ya vituo 80 vinavyotumia vifaa vya mionzi viwandani, maabara hii itsaidia kuhakiki vifaa hivyo na kuongeza ubora wa bidhaa zinazizalishwa nchini , kusaidia uchumi kupitia mchango wa teknolojia na nyuklia katika sekta ya Afya kilimo , mifugo barabara,maji na usimamizi wa watu na mazingira mara uchimbaji na usafirishaji wa madini ya urani utakapoanza

Aidha Busagala ameiambia Kamati hiyo kuwa maabara zilizopo sasa zinauwezo wa kupima sampuli 800 za mazingira kwa mwaka, ambapo kuwepo kwa maabara changamano kutasaidia kupima sampuli 3000 za mazingira ambapo matokeo yake yatasaidia kuongeza taarifa za kiusalama za mionzi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge huduma na Maaendeleo ya jamii Stanslaus Nyongo aliishauri TAEC kuendelea kumsisitiza mkandarasi kukabidhi jengo kwa wakati kama alivyoahidi ili kazi za maabara,ziendelee kama zilivyokusudiwa Sambaba na hilo amewataka kuhakikisha kuwa maabara ya Dodoma ziendelee kufanya kazi kwani ujenzi wkae umeshafikia 85% jengo kukamilika.

Mwenyekiti wa Bodi ya 
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Prof Joseph Msambichaka ameishukuru kamati hiyo na kusema kuwa maelekezo yote waliyoyatoa kwao wameyachukua watayafanyia mjadala,na menejimenti watayachambua na kutoa mapendekezo ambapo kuyarudisha mrejesho kwa Wizara ambapo watafanya mawasiliano na Kamati
 Mkurugenzi Mkuu wa TAEC Prof.Lazaro Busagala akitoa ufafanuzi wa Kamati ya kudumu ya Bunge huduma na Maendeleo ya Jamii

Mkurugenzi Mtendaji wa TAEC Prof. Lazaro Busagala akizungumza na Kamati ya kudumu ya Bunge huduma na maendeleo ya Jamii hawapo pichani

Post a Comment

0 Comments