Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZALISHAJI JENGENI NGUVU YA PAMOJA YA USHIRIKA KUYAFIKIA MASOKO EAC

Na Ahmed Mahmoud
Watanzania hususani Wanaushirika wameaswa kupigania umoja wao
utakaosaidia kuleta maslahi ya wazalishaji na kuyafikia masoko ndani
ya Jumuiya ya Afrika mashariki badala ya kuwanufaisha wafanyabiashara
wakubwa pekee.

Akizungumza katika Jukwaa la kwanza la Vyama vya ushirika vya nchi za
Afrika Mashariki linaloendelea jijini Arusha Mwenyekiti wa Shirikisho
la vyama vya ushirika Tanzania TFC Charles Jishwili amesema lengo kuu
la Jukwaa hilo ni kuona namna nzuri ya kubadilishana uzoefu ili
kuwanyanyua wazalishaji.

Amesema Kwamba Sekta ya wanaushirika katika Jumuiya hiyo ina fursa
kubwa kuweza kuwainua wazalishaji kwa kujenga masharikiano na masoko
ya wao kwa wao ili kuweza kuwanufaisha badala ya kutengenezea mtu moja
kujinufaisha.

Amesema kwamba Msingi huo wa kuwashirikisha wazalishaji utapelekea
Mataifa hayo na serikali kuweza kuongeza wigo mpana wa kuufanya
ushirika kuweza kusaidia kujenga Taifa na mataifa yetu kwa msingi na
uzoefu wa wenzetu Kenya.

Awali akiongea Mrajisi Msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Morogoro
aliemuwakilisha Mrajisi wa vyama  vya ushirika nchini Kenneth Shemdoe
amesema Muungano huo umekuja wakati muaafaka na umeisaidia serikali
kuweza kupata uzoefu na kujifunza  Jinsi nchi jirani zimefanikiwa
katika kada hiyo.

Amesema kwamba Taifa la Kenya limeweza kupiga hatua na kusaidia
wazalishaji katika sekta ya ujasiriamali na kilimo kuweza kufanya kazi
zao na kupata faida jambo ambalo kwetu tunahitajika kuusimamisha
ushirika uweze kuongoza uchumi wa taifa letu.

“Sekta ya kilimo Imepiga hatua kubwa lakini Jukwaa hili limetusaidia
kuweza kujua kwamba vyama vya ushirika ni msingi mkubwa na jukwaa la
maendeleo kwa biashara za nchi zetu na Afrika mashariki”

Nae Mtendaji Mkuu wa Muungano wa vyama vya ushirika nchini Kenya
Daniel Marube amesema kwamba ipo haja kwa Serikali na Wakuu wa nchi za
mataofa ya Afrika mashariki kuona umuhimu wa kuzinyanyua sekta za
vyama vya ushirika na kuzipa meno kwa maendeleo ya Mataifa na biashara
baina ya wazalishaji wenyewe bila kutumia wafanyabiashara ambao
wamekuwa wakijinufaisha

Amesema wameweka maazimio ya kuhakikisha ushirika unamnufaisha
mazalishaji wa chini kwa kiwango ili aweze kutumia soko la Jumuiya
mafano hapa Tanzania tumekuja kufanya mazungumzo na wazalishaji wa
mashudu ya alizeti na pamba sanjari na wao kununua maziwa na mitamba
ya kisasa kutoka nchini humo.


 

Post a Comment

0 Comments