Ticker

6/recent/ticker-posts

MATATIZO YAWAKUTANISHA VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA EAC

 


 Viongozi wa vyama vya ushirika kutoka nchi za jumuiya ya Afrika ya mashariki wakutana jijini Arusha kwa lengo la kujadili fursa na changamoto  zinazozikabili vyama  vya ushirika kutoka nchi wanachama ili kuweza kuweka mikakati ya kudumu ya kuhimarisha vyama hivyo.


 Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa shirikisho la vyama vya ushirika kutoka nchi za jumuiya ya Afrika ya mashariki kupitia  (EAFF),Mkuu wa wilaya ya Monduli Frank Mwaisumbe amesema jukwaa hilo la viongozi hao litasaidia upatikanaji wa fursa za ajira pamoja na kuongeza pato la Taifa.


"Ni dhamira ya serikali za nchi wanachama wa EAC kuandaa mazingira wezeshi wa ustawi wa  ushirika na kutumia mfumo wa ushirika kuwezesha wananchi kiuchumi na kijamii kwa lengo la kuhimarisha masoko na uwekezaji katika viwanda na sekta ya fedha,"amesema Mwaisumbe.Aidha Mwaisumbe amesema kuwa uzoefu wa viongozi hao katika majadiliano hayo utaenda kuhimarisha huduma kwa wanachama ambapo utakwenda kuongeza pato katika jumuiya ya Afrika mashariki.


"Na wananchi wa jumuiya ya Afrika ya mashariki zaidi ya milioni tatu hutumia bidhaa za mashambani zinazozalishwa na kusimamiwa na vyama vya ushirika kwani hali hiyo inatokana na usimamizi mzuri wa serikali zetu za jumuiya ya Afrika ya mashariki,"amesema.Naye Katibu wa vyama vya ushirika Tanzania,Alex ndikile amesema kupitia kongamano hilo nchi ya Tanzania itapata manufaa ya fursa za kibiashara na ajira ambapo kupitia vyanzo vya mapato vya ushirika wataweza kwenda kusimamia uchumi wa Afrika ya mashariki kwa pamoja.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa vyama vya ushirika nchini Kenya, Silas Maguti amesema kongamano hilo linaumuhimu katika jumuiya ya Afrika ya mashariki kwani litawasaidia katika kutembea pamoja katika uzalishaji nakuwa na sauti moja katika vyama vya ushirika.

Post a Comment

0 Comments