BREAKING NEWS

Sunday, February 6, 2011

AFC YAPETA YACHAPA RUVU SHOOTING

Timu ya AFC ya jijini hapa ambayo ilikuwa inashikilia mkia katika mashindano ya ligi kuu yanayoendelea katika viwanja vingi nchini hapa jana imeweza kurejesha nguvu mara baada ya kuweza kuwanyuka mkwaju 1-0 timu ya Ruvung Shooting mechi ambayo ilichezwa katika kiwanja cha Sheikh Amri Abeid uliopo jijini hapa.

Timu hii ya AFC ambayo imefululiza kufungwa katika mechi mbalimbali zikiwemo za nyumbani na nje ya nyumbani imekuwa ikikabiliwa na matatizo mengi ikiwemo la kususiwa na washabiki kutokana na kufululiswa kufugwa .

Katika mechi hii ambayo imeweka historia kwa wakazi wa mkoa wa Arusha hususa ni mashabiki wa mpira wa mkoa huu ilikuwa kali ya kuvuta nikuvute baina ya wenyeji ambao ni timu ya AFC pamoja na wageni ambao ni Ruvu shoting mechi ambayo hadi kumalizika kipindi cha kwanza hamna ata timu moja ilikuwa imeona nyavu.

Waliporudi kipindi cha pili wachezaji wa timu ya AFc walionyesha mabadiliko Fulani kwani walikuwa kwa kasi kubwa ya kutaka kushinda na kuondokana na kaz a ya kushuka daraja hali iliyosababisha ilipotimu kunako dakika ya 54 ya mchezo mchezaji aliyejulikana kwa jina la Shingwa Mshingwa aliweza kuiandikia timu yake bao la kwanza mara baada ya kupokea pasi kutoka Abudala Juma goli ambalo liliwainua mashabiki ambao walikuwa wamekuja kushuhudia mechi ile na kuwafanya warudishe moyo wa kuipenda timu yao ya mkoa.

Mara baada ya timu hii ya AFC kufunga goli liliwaliongeza kasi ya kutafuta magoli mengine pamoja na kuwakaba vilivyo wachezaji wa Ruvu Shooting hali iliyosababisha hadi kipenga kulia AFC kuibuka kidedea na kujiongezea pointi na ambazo mpaka sasa zimewafanya kufikia point inane.

kocha wa timu ya AFC Rashid Chama naye alisema kuwa anashukuru mungu kwa ushindi ule na anahamini kuwa bado wanayo nafasi ya kushinda na kuwa anawaambia washabiki wa mpira wa mkoa wa Arusha kuwa AFC haitashuka daraja.

Alisema yeye amekabidhiwa timu hivi karibuni na alipokabidhiwa timu walikuwa hawajafanya zoezi hata siku moja na hivyo ndio sababu kubwa iliyowafanya wao kufungwa.

“unajua mimi nimekabidhiwa timu hatujafanya hata zoezi wachezaji wengine wamekuja siku ambayo mechi ndo inachezwa kwanza wamechoka pili hawana mazoezi kweli hapo tukifungwa tutalalamika “alisema Chama.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates